
LOML | Love Of My Life (201)

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:201
Alitabasamu na kusema “kwa upande wangu mimi ni historia tu ya maisha yangu. Bibi yangu analipenda sana kanisa lile ingawa kila mahali kuna kanisa. Baada ya kuhamia kwake nilijikuta nakwenda na bibi kanisani Mara nyingi sana.
Kanisani pake palianza kuwa nyumbani kwangu. Nikilia, nikiwaza wapi nimekosea, nikiumia, nikifanya lolote basi kanisa lile ndiyo kimbilio langu.
Hata nikazoea kabisa. Nikiwa pale ninakuwa na furaha sana. Nafurahia kıla kitu ni kama huwa naongea na Mungu kabisa. Unajua kinacho nivutia zaidi?”
Nilitabasamu na kusema “eenh Nipe siri.”
Alitabasamu na kusema “ni lile grotto pale. Pana Siri zangu nyingi sana pale. Napenda kila kitu.”
Nilitabasamu tu na kusema “unakuwa mzuri sana ukifurahi unajua.”
Alinitazama akitabasamu na kusema “unanifanya nafurahia sana Ricky.”
Nilitabasamu na kusema “karibu sana.”
Akaniuliza kwa upole “na wewe Unaendeleaje?”
Nilishusha pumzi na kusema “naendelea vizuri sana, lakini nachoka sana hapa nilipo natamani sana kujilaza.”
Alitabasamu na kusema “ni vizuri ukajilaza ili mwili ukae vizuri na hutakiwi kujitesa kwa mawazo hata kidogo. Kunywa dawa na vipi ushakula?”
Nilitikisa kichwa na kusema “bado kipenzi, lakini Nina hakika sio muda nitakula.Tutakula wote.”
Alitabasamu tu, na wakati huo mama Babuu anatoka na vitu akisema “Boss unaweza kwend tayari.”
NIlimshika mkono Pina na kusema “tunaenda wote?”
Alitabasamu na kusema “bila Shaka.”
Başı kWa upendo tuliongozana mpaka chumbani.Tulipofika, alisimama katikati ya chumba akisema “waoooo!!, pananukia vizuri sana.”

