
LOML | Love Of My Life (202)

ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:202
Nilitabasamu na kusema βsana Pina, sana na pamependeza.β
Pina alitabasamu na kusema βwaoooo!!, ni pazuri sana, eenh niambie pamendeza sana.β
Nilitabasamu na kusema βsana Mpenzi.β
Alianza kama kunipapasa, hapa ndiyo nikatoa fimbo ambayo nilikuwa nimeishikilia mimi na kusema βhii ndiyo zawadi yako.β
Nilimpatia mkononi na kusema βmimi nikiwepo huna sababu ya kutumia. Nikiwa mbali na wewe utatumia fimbo hii. Ni nzuri sana, Ina fanana sana na wewe, halafu Ina ngβara vizuri sana.β
Pina ni kama sijui nimempa kitu gani kwa furaha ile. Alikuwa anaishika shika ile fimbo akisema βbaby ni nzuri sana, tazama inavyo teleza. Ni nzuri sana yaani, nimefurahi sana.
Natamani uone namna nimefurahi Mungu wangu, Ricky umenikumbuka jamani. Sistahili this love, baby wewe ni mwanaume unayejali sana. Tazama, ona ilivyo nzuri.β
Nilimsogelea na kusema βnitafanya kila kitu kuhakikisha unakuwa na hii furaha maisha yako yote. Utakuwa na furaha hii hii. Karibu sana Pina.β
Pina alinikumbatia kwa nguvu, hata nilimbeba na kuanza kuzunguka naye, Kisha Tulijikuta tumeangukia kitandani. Alikuwa juu yangu, na mimi nilikuwa chini, nikawa namtazama namna alivyo mzuri, alikuwa ametulia tu.
Kisha nilimbusu taratibu midomo yake mizuri, alinibusu pia na Kisha tulijikuta tunacheka. Tulicheka huku Pina alisema βmimi ni mzito sana, nilisahau mgonjwa wangu hana nguvu kabisaa.β
Nilicheka nikisema βhuna akili ujue, utakuja kuniua mimi.β

