
LOML | Love Of My Life (204)

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:204
Mama Babuu alitabasamu tu. Na Baada ya hapo mama Babuu alisema “karibuni sana chakula.”
Akawa anaondoka, wakati anaondoka Pina alisema “mama, mbona una ondoka. Tule wote mama!!”
Mama Babuu alishangaa na kunitazama, nilimtazama na kusema “walau uache ubishi mama Babuu.”
Alitabasamu na Kisha Pina alisema “kula pamoja ni vizuri sana, tunamuabisha shetani ambaye Mara zote hapendi umoja wa familia. Tusali tule.”
Başı alisali sala nzuri sana, nakumbuka baadhi ya maneno “chakula hiki kikawe dawa kwetu, dawa ya kutupa kiu ya kukujua vizuri. Mbariki aliye tafuta chakula hiki kamwe asipungukiwe ghalani kwake, Batılı aliyepika na mbariki kila anayekula. Asile tu kama chakula, Bali ale kama dawa mpya ya maisha yake. Amen.”
Mimi na mama Babuu tulitabasamu, na Kisha nilisema “Karibuni sana chakula, karibuni.”
Nilianza kula, ulikuwa mchemsho wenye viazi ndani yake. Nilipokula kijiko cha kwanza. Unajua mchesho sio maji yamejaa hapo. Huu mchezo una mambo mengi sana. Nilimtazama mama Babuu na kusema “mama Babuu huu mchemsho!!!”
Mama Babuu alicheka na kusema “nilijua tu utasema, kusema ukweli hata mimi nimeomba darasa kwa madam Pina. Yeye ndiyo Kapika.”
Nilishangaa na kusema “Unataka kuniambia Pina uliniacha chumbani ukaingia jikoni?”
Pina alitabasamu tu na Kisha Niliendelea “nimeamini, ile jana nilijua umesafiria nyota ya bibi kumbe hapana.”
Pina alicheka na kusema “kupika ndiyo kitu kingine napenda zaidi. Umependa kweli mpenzi?”
Nilitabasamu badala ya kujibu nikala tena, nikala tena na tena halafu nikasema “hapa lazıma nipone, ni tamı sana, ni tamu mno.”

