
LOML | Love Of My Life (206)

๐๐๐๐ (๐ณ๐๐๐ ๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐) โฃ๏ธ:206
Pina alitabasamu, na Kisha mimi na baba tulitazamana tu. Nakumbuka, Pina aliendelea kula. Baba yangu alisema โnimekubali, Mara nyingi mtu anayefanya kosa ni ngumu sana kukubali.
Ataonekana yeye ndiye kakosewa na aliyekosewa ndiye mkorofi. Sijui kwanini sikujua uhalisia wa Yule binti mapema. Mimi kila nikimuwaza pumzi haitoshi.โ
Nilitabasamu na kusema โsasa hivi ndiyo naelewa baba. Ilikuwa lazima tuone ubaya wake wote ndiyo maisha mengine yaendelee.
Mimi sijali atasema nini baba, unajua nilimkuta hapa. Nimemtimua ndiyo hayo machozi. Mama ana haki ya Kuwa hivyo ana mtetea mkwe wake. Subiri siku akijua itakuaje.โ
Baba alianza kula, alikula akiendelea kuzungumza kuhusu Gabby, na mwisho alisema โhuu mchemsho siwezi kushiba, nakula sijui hata unaenda wapi. Ni mtamu sana. Ningekuwa nakula hivi kila siku ningekuwa sio mtu wa kawaida.โ
Nilicheka tu na kusema โPina huyo baba.โ
Baba alisema kwa kushangaa โBinti yangu unajua kupika namna hii?, mtafanya nihamie kwenu sasa.โ
Tulicheka sana, baba yangu ana furahisha sana na alivyo utasema haongei Ila maneno yake yananiacha hoi. Tulikula pale tulimaliza. Pina alianza kuondoa vyombo nikamzuia. Na kuita โmama Babuuu!!โ
Alifika na nikamuomba amsaidie Pina. Ni kweli anaweza kufanya kila kitu. Lakini kwa hali yake kuna mambo anafanya kwasababu tu hakuna msaada lakini hapa kwakuwa kuna msaada atulie, hawezi kufanya yeye kila kitu.Lazima asaidiwe haiwezekani ataseke.
Mama Babuu aliondoa vyombo Kisha niliona wananongโonezana. Baada ya muda Pina alisimama na kusema โnaomba nikapumzike kidogo niwaache mnazungumza.โ
Nilitabasamu na kusema โNaomba nikupeleke mamaa!!โ
Pina alitabasamu, Kisha mama Babuu aliendelea na mambo yake huku mimi nikimwambia baba yangu โnarudi baba, narudi.โ
NAAAAAAAM HUU NDIO MWISHO WA SEASON FOUR
HONGERAAAA, UMEBAKISHA SEASON MOJA TU!

