LOML | Love Of My Life (208)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:208
Nilitabasamu, na baba pia. Başı baba aliniambia β€œukimaliza mambo yako La huyu msichana.”

Nilitabasamu, niliongea mengi na baba yangu na hata kuhusu mtoto wake. Baba alikuwa anafurahia kila kitu aliniambia β€œMungu amekupa mtoto kwa namna ya pekee mwanangu. Fanya kΔ±la kilicho ndani ya uwezo wako. Hii ndiyo familia yako sisi tutakuwa mbali na nyie.

Mpende anavyo paswa na mpe furaha anayotakiwa kuwa nayo. Akiwa na furaha na mtoto wake atakuwa na furaha na atakufanya kuwa baba. Kuwa baba sio lazΔ±ma uzae wewe.

Kuna baba mlezi wazuri sana. Nakuamini mwanangu utakuwa baba mzuri sana kwake na mtoto wake. Mungu akupe uzao wa kutosha na nipate wajukuu wengi kwa jina langu.”
Nilitabasamu na kusema β€œAmen baba yangu, Amen.”
Tuliongea mengi sana na zaidi baba yangu aliaga na kuondoka zake.

Wakati baba yangu hajafika hata mbali mimi nikiwa nimekaa natabasamu, nakumbuka maneno ya baba yangu kuhusu Pina, kuhusu maisha yangu natabasamu tu. Baba yangu ni mtu mzuri sana kwenye maisha yangu.

Ni mtu ambaye anasimama na mimi kwenye kΔ±la namna kuhakikisha tu nakuwa salama. Nilikuwa na furaha tu, mwili wangu ingawa haukuwa na nguvu lakini walau nilikuwa naweza kutabasamu na nilikuwa ninao uhakika kuwa nitakuwa na furaha na nitaendelea vizuri kabisa.

Ndani yangu amani ilikuwa kubwa sana kwasababu Pina yupo kwangu, Hakuna mtu atamchukua kutokea kwangu. Başı nikikumbuka ladha ya chakula chake, tayari najiona kabisa mimi bila huyu love of my life, maisha yangu sitaweza kupumua kabisa.

Nilisikia hodi nikajua baba amesahau chochote kitu, si nikainuka kwenda kufungua. Vile nafungua tu nakutana na shemeji yangu mke wa Max. Nilishangaa kumuona hata nilisema β€œooh shemeji karibu sana.”

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

SIMULIZI YA INGIZA FULL

SHEM MI NATAKA FULL