
LOML | Love Of My Life (209)

๐๐๐๐ (๐ณ๐๐๐ ๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐) โฃ๏ธ:209
Alitabasamu na kusema โnashukuru sana shemeji.โ
Aliingia ndani, nikamuuliza anachohitaji na mama Babuu alimuhudumia. Wakati anapata zake juisi nilimtazama na kusema โkwema shemeji, karibu.โ
Alinitazama kWa upole na kusema โshemeji yangu, sijui kitu Gani kimetokea kwenu lakini nakuomba kwaajili ya maisha ya watoto na mimi mrudishe mume wangu kazini. Nimeumia kuona kuwa mume wangu hafanyi Tena kazi na wewe na hakuna sehemu anapata.
Shemeji maisha yamekuwa magumu sana kwetu. Nikaona nije hapa kwa niaba yake kuomba msamaha kwa maana hata sijui ni wapi amekosea.โ
Maskini ya Mungu, mwanamke huyu angejua mume wake alichofanya kwa mke wangu. Mimi na yeye tumesalitiwa asingekuwa hapa kumuombea msamaha. Lakini kwakuwa hajui acha afanye wajibu wake kama Mke na mimi kutoka ndani ya moyo wangu ndoa yake hainihusu, Mungu peke yake ndiye atakayemnyoosha akae kwenye mstari.
Nilimtazama shemeji yangu nikamuuliza โunajua alichofanya?โ
Shemeji yangu alinitazama na kusema โhapana shemeji, haniambii kitu chochote.โ
Nikamuuliza tena โanajua kuwa upo hapa?โ
Bado alinijibu โhapana, hajui chochote kile ni mimi tu nimeamua kujiongeza.โ
Nilishusha pumzi na kusema kwa upole โshemeji yangu, siku nyingine usirudie kumuombea mtu msamaha kwa kosa ambalo hulijui kabisa.
Usibebe msalaba wa mtu ambaye amejitakia mwenyewe. Yeye mumeo anajua alichofanya kwangu, anaelewa kosa lake na hayupo tayari kutubu na badala yake yeye mwenyewe ameacha kazi. Mimi sijamfukuza kazi.
Lakini ukweli ni kuwa hata kama angebakia, kwa kitendo amenitende ni kuwa hastahili msamaha wangu. Ningemfukuza, amejiwahi.Na hata nikimsamehe hawezi kuwa karibu tena hata kuwa sehemu ya biashara yangu haiwezekani. Mungu atamsaidia atapata tu kazฤฑ mahali pengine. Na kuhusu wewe shemeji au watoto ukiona nafaaa kukusaidia kwa chochote nyumbani unapafahamu au kazini kwangu unapafahamu.โ

