
LOML | Love Of My Life (211)

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:211
Başı nilisogea kitandani na kujilaza karibu na mpenzi wangu, alivyo kuwa amelala kazuri kama katoto. Niliita kWa upendo “baby!!, mpenzi wangu, my fortune, tafadhali amka.”
Niliona taratibu alifungua macho yake akitabasamu. Na mimi nilitabasamu na Kisha nilisema kwa upole “nashukuru sana kwa chakula kizuri sana Pina. Nimefurahia sana na Nimekula sana. Chakula ni kitamu naona kabisa nikila na baadaye kesho naamka na nguvu kabisa. Mtoto unanichanganya mimi.”
Alitabasamu na kusema “thanks for the compliments sweetheart. Nimefurahi sana hata Umenifanya nitafakari tena kitu gani kizuri nikipika utafurahia.Nakupenda Ricky.”
Nilitabasamu na kusema “wewe unajua kipenzi, ukipika chochote niamini kitakuwa hi kitamu sana. Nashukuru.”
Alinikumbatia, kıla akinikumbatia nasikia rahaa sana. Unajua Kumbe ni tofauti sana.
Ukiwa na mtu unayempenda ukimuona tu unatabasamu, ukiwa naye karibu unatabasamu, akikuambia maneno mazuri na matamu unasisimuka bila sababu, akikukumbatia unaishiwa nguvu zote, akikubusu unatetemeka, namaanisha hivi ukiwa na mtu unayempenda kuna furaha ambayo sikuwahi kuwa nayo zamani, kuna furaha sijawahi ipata maishani ndiyo kwa Mara ya kwanza na furaha hii inanishangaza sana. Ni furaha ya kweli, furaha kutoka ndani ya moyo wangu.
Mpenzi wangu Pina aliniambia “najua unajisikia vizuri sasa, naomba niruhusu nirudi nyumbani.”
Nilimtazama nikisema “ninakupeleka, tunaenda wote.”
Alitabasamu, halafu aliniambia “lakini si unaumwa wewe.”
Nilimtazama na kusema “abiria chunga mzigo wako.”
Alicheka akisema “yaani wewe na hapo ni unaumwa hivyo.”
Alitabasamu na kufanya na mimi nitabasamu.

