
LOML | Love Of My Life (213)

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:213
Kiukweli Hali yangu ilikuwa tete, Ila nitafanyaje sasa, ilikuwa tu ni lazıma nijishikilie Ila natamani hiyo siku ifike, hiki kitanda nilale na mwanamke huyu ninayempenda sana. Naona kabisa sitaamka mimi. Maana hapa tu ninasikia raha ajabu.
Nilimtazama na kusema “asante kwa kuja kwenye maisha yangu Pina. Unanifanya nijisikie amani na furaha muda na wakati wote.”
Alitabasamu na kusema “uwepo wako kwenye maisha yangu una maana zaidi ya kıla kitu kwenye maisha yangu. Nitafanya kila kitu nisikukose maadam najua wewe ni wangu, unanipenda. Niambie Ricky Unanipenda?”
Nilitabasamu na kusema “Nakupenda mno na nitakupambania.”
Alitabasamu na kuniambia “kwa Mara ya kwanza napata furaha kwenye maisha yangu. Nakuahidi sitakuacha uende, nitakupigania.”
Nilicheka, Akacheka pia. Nilimtazama pale ukutani na kusema “wiki hili ratiba yangu itakuwa ngumu kidogo lakini jiandae muda na wakati wowote nitakufuata wewe na Samweli tukatembee kidogo.”
Alinitazama na kuniuliza “umesema na Samweli?”
Nilitabasamu nikisema “tuondoke sasa, tunachelewa.”
Akaniuliza “unaendesha wewe?”
Nilicheka nikisema “kama unataka nikumwage sawaaaa.”
Tulicheka, tulikuwa tunasema hivyo kwa maana, kwa maana sikuwa na nguvu bado lakini sio nguvu za kubusu hizo kwenye kumbusu Pina zimejaa.
Başı nilichukua na simu ya Gabby nikaweka mfukoni. Sikuwa najali Nani kapiga wala nani kamtafuta sikutaka kuhangaika nayo tena. Tuliingia kwa gari, Yule dereva wangu wa kazini ndiyo ilikuwa aendelee na mimi tu mpaka nikae sawa maana kikawaida napenda kujifanyia mambo yangu mwenyewe. Tulikaa nyuma. Sasa ukimuona Pina ameniegemea, nilikuwa nasikia raha sana.

