LOML | Love Of My Life (215)

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:215
Nilitaka niseme kama hujisikii hivi ambavyo mimi nina jisikia na huyu mwanamke başı hupendwi kumbe Kuna watu kwao kuteseka ndiyo mapenzi nyie siwezi waambia lolote.

Unajua kuna wakati ninavyo jisikia natamani wote wote bila kujali cheo chako niwatafute sehemu yenu ya kuishi halafu hii hapa nimpe Pina wangu tu ajinafasi hatakiwi kusumbuliwa kwa raha anazonipa.Lakini ndiyo siwezi, tukibaki wawili nyie mtajifunza wapi kupendana kama sio hapa.Itabidi tu mbaki na sisi hapa, mshuhudie upendo wa kweli.

Tulifika mpaka kwao, Baada ya kufika tulikuta bibi na Samwel wamekaa nje na mambo Yao wenyewe hawana habari. Samwel anampenda sana mama yake alimkimbilia kama alivyo fanya Mara ya kwanza nimefika hapa.

Nilikuwa nafurahia tu walivyo hata mama yake alisema “mbona husalimii.”
Mtoto huyu alinisalimia, nami niliitikia kwa upendo nikisema “hujambo Şam.”
Alitabasamu na kusema “Sijambo, asante kwa kumrudisha mama yangu.”
Nilitabasamu na kusema “lazıma nimrudishe salama kwasababu mimi pia ni mama yangu.”

Sam alishangaa na macho yake kubadilika akisema “mama yako?, hapana huyu ni mama yangu mwenyewe.”
Nilicheka na kusema “ni mama yangu pia.”
Akaniuliza kWa upole “kwahiyo mimi ni kaka yangu wewe?”

Nilitabasamu na kusema “ni kweli kabisa.”
Nilimtazama Pina, alikuwa na furaha sana. Tulisogea mpaka kwa bibi, bibi alinikaribisha kwa furaha sana. Nilimsalimia kwa heshima na Şam alimsimulia bibi kuwa mimi ni kaka yake, tukacheka. Pina alisema “Bibi anaitwa Rodricky, ndiye niliyekuwa nakuelezea kuhusu yeye.”

Bibi alitabasamu na kusema “karibu sana mjukuu wangu.”

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata