
LOML | Love Of My Life (219)

πππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:219
Nilitabasamu na kusema βhuu sio muda wa kumtafuta mchawi nani, na sipo hapa kukufundisha namna ya kuishi. Giana umeniangusha sana, kama dada umeniangusha.
Nilikuwa nakutegemea sana, nilikuwa nakuona kama mwalimu mzuri kwetu, nilikuwa nakuona mwanamke wa busara sana na badala yake umejivisha kivuli kisicho kufaa.
Kizazi chako kitafuata haya hata kama hawakuoni Ila kwasababu roho ina tabia ya kufuatilia na shetani Ana tabia ya kutumia udhaifu kukufanya wake siku zote utateseka.
Nakuonea huruma sana kwasababu wewe ni wa busara sana. Mithali 31:30 inasema Kujipamba ili kuvutia ni udanganyifu, na uzuri unapita upesi; bali mwanamke anayemcha BWANA atasifiwa.
Na bado tena neno linatuambia kuwa Mithali 28:13 Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.
Giana bado unayo nafasi ya kurudi miguuni kwa Mungu wako, kuombea ndoa yako, kutubu dhambi zako na kuanza upya. Unayo nafasi hiyo, unayo Giana.
Simamia ndoa yako, kwenye haya maisha sio kΔ±la unaye furahi naye ni mtu mzuri wengine wapo kwaajili ya kukuharibia maisha na familia yako. Mimi naenda, kwaheri.β
Wakati naondoka tu nikasikia mume wake anasema βwifey, tuna mgeni?β
Giana alijibu βYes babe, ni Shem alileta simu ya Gabby, lakini ndiyo anaondoka.β
Alishtuka na kuuliza βSimu ya Gabby?.β
Mkewe aliuliza βkwani kuna tatizo?β
Nilitabasamu na kusema βvipi kaka, usijali Giana ilikuwa inapigwa sana, ilikuwa na meseji nyingi nimeifunga utamwambia tu apitie.β

