
LOML | Love Of My Life (221)

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:221
Akiongea kizungu chake kwa upole sasa mimi natabasamu, nilimwambia “nipo hapa mama, unataka kusikia nini kutoka kwangu.”
Pina aliniambia “sauti yako, sauti yako ni sababu ya maisha mapya kwangu, I love the way you talk, haswa ukisema nakupenda Pina wangu, nachanganyikiwa.”
Nilitabasamu na kusema “Nakupenda Pina wangu.”
Akakaaa kimya, nikaita “Pina!!, Pina!!, Pina unanisikia.”
Akacheka na kusema “nilishachanganyikiwa uliposema Nakupenda Pina wangu.”
Nikacheka nikisema “hivi unajua akili huna Pina.”
Alinijibu kwa upole “kwaajili yako Ricky, kweli sina akili, Sina kabisa, crazy for you baby boy!!”
Nilitabasamu na kusema “Pina madeko wangu, napenda ukideka, unanikumbusha kuwa mimi ni mwanaume na natakiwa kukudekeza zaidi. Lakini sasa, ukisema Nakupenda Ricky wangu ndiyo nachanganyikiwa.”
Alicheka na kusema “Loml, nakupenda sana.”
Nilicheka nikisema “Pina sitaki, Loml ni yangu, umeniibia, umeniibia ni yangu hiyo.”
Pina alicheka akisema “una hati miliki
Yake, ni yangu na nishasajili kabisa.”
Hapo nishafika nyumbani tupo tunagombaniana Hati miliki ya LOML ni ya nani. Na wote mnajua ni yangu sema tu Pina ni mkorofi. Başı tunacheka mpaka naingia sebuleni ni fujo. Nilimtazama Willy huku natabasamu nikasema “LOML.”
Pina akasema “Sitaki ni yangu mimi ndiyo nikuite hivyo.”
Nikacheka na kusema “acha utoto Pina, ujue Willy yupo hapa anatuona hatuna akili. Nitakupigia sawa My Fortune.”
Pina alisema “no no nooooo no no hii ndiyo naimiliki kabisa.”

