LOML | Love Of My Life (226)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:226
Nilimpigia Pina na kusema β€œLoml, mimi ndiyo napata muda sasa. Naweza kukuona kweli?”
Pina alisema β€œhaki ya Mungu Ricky walau nikuone hata kidogo tu nimekukumbuka sana.Nitashindwa kulala, nakumiss eti.”

Nikatabasamu tu na kusema β€œnakuja.”
Basi nilipita supermarket. Nilinunua vingi kwaajili ya mahitaji ya nyumbani. Nikaweka kwa gari na safari ilianza. Nilipofika nikampigia simu, alitoka nami nikampokea kwa furaha akaingia ndani ya gari. Alinikumbatia akisema β€œI missed you so very much.”

Nilitabasamu na kusema β€œmimi zaidi mpenzi.Lakini naomba vumilia, kuna mambo nafuatilia na kazini sasa mambo yamekuwa mengi sana. Nakukumbuka muda wote lakini nakuwa sina namna. Niombee suala la taraka liende vizuri na kazini nako mambo yazidi kuwa mazuri.”

Alitabasamu na kusema β€œamen mpenzi, asante kwa kuja kuniona.”
Nilimbusu na kusema β€œnimekuwa na siku ngumu sana. Naomba niende sasa ila kuna mzigo wako hapa.”

Basi alitabasamu tu nilimshushia vitu na kusaidia kubeba. Akawa ananishangaa tu, kisha nilimpa pesa mkononi na kumbusu nikisema β€œtutawasiliana mpenzi wangu nakupenda.”
Aliniambia kwa upole β€œRicky Nakupenda.”
Nilitabasamu tu.

Kabla sijafika hata nyumbani alinitumia ujumbe β€œthanks for taking care of me and my family.”
Nilitabasamu tu, anaweza walau kuniandikia ujumbe japo sijui namna gani anateseka. Ingawa najua kuna watu wenye macho simu za button hata akifumba macho hakosei. Nilimpigia akawa hata anataka kulia basi tunacheka hata nilifika nyumbani.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

CHAGUO LA MOYO FULL

TOBO LA PANYA FULL

BIKIRA YA BIBI HARUSI FULL