LOML | Love Of My Life (23)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:23
Nilimtazama na kusema β€œnisamehe mke wangu, nakupenda sana na nitakuwa mwangalifu sana.”
Mke wangu alinitazama, halafu alitaka kushuka, akakunja sura akisema β€œMungu wangu!!!, Mungu wangu!!, naumia sana Ricky, siwezi kukaa vizuri panauma.”

Alinifanya nizidi kuumia, nilijikuta natokwa na machozi kabisa. Hata nilisema β€œmke wangu nifanye nini uwe sawa?”
Mke wangu alinitazama na kusema β€œnaomba tu pain killer tafadhali.”

Mtoto wa watu nilianza kufuata dawa na nikarudi na kumpatia. Alikunywa, kisha nilimchukua taratibu mpaka bafuni. Natamani ungemuona mke wangu siku hii. Hata sikuwa na hamu, nilikuwa najisikia kuumia muda wote, naona kama mimi ndiyo mtenda dhambi dunia hii hakuna mwingine.

Kufanya mapenzi kinyume na maumbile ni dhambi ambayo mimi kama kijana ambaye nimelelewa na kutunzwa vizuri na baba na mama yangu nilisema kamwe, katu sitakuja nikae nikaifanya. Naumia imenitokea bila kujua kivipi na tena na mke wangu naumia najisikia vibaya sana.

Mke wangu alikosa raha kabisa tangu hii siku. Nilikuwa najitahidi kumletea zawadi ananipokea akisema β€œweka tu hapo.”

Namtazama kwa huruma namuuliza β€œunajisikiaje baby, mke wangu au unajisikia vibaya twende hospitali nipo tayari kuwajibika na hili.”

Mke wangu ananitazama na kusema β€œhapana mume wangu sijisikii tu vizuri, najisikia vibaya sana.”
Nilikuwa namkumbatia huku neno samahani ya dhati ikitoka kwenye uvungu wa moyo wangu. Na hapo nakaa kitandani namuacha ana chat na rafiki yake hata wataongea video call mimi tena natoka zangu naenda sebuleni au nje.

Hili tukio, lilinifanya mara kwa mara niongee na Mungu nikisema β€œMungu naomba nisamehe sana halikuwa lengo langu, haikuwa nia yangu, nisamehe sana Mungu wangu.”

Natamani nikuambie nilivyokuwa nateseka, hata nikawa natazama jinsi ya kumsaidia mwanamke aliyeingiliwa kinyume na maumbile kwa mara ya kwanza ili ajisikie vizuri kiakili na kimwili.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata