
LOML | Love Of My Life (235)

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:235
Leo nataka tukeshe mpenzi, nataka tufurahie mwanzo wetu mpya. Unajua siwezi kuacha utamu huu mpenzi. Naomba tukaoge halafu nikuoneshe kiti gani kingine naweza kufanya kwaajili yako.”
Nilitabasamu na kumuuliza “ina maana mama, unataka kuniambia kuna zaidi ya haya. Si utaniua mwenzio.”
Alitabasamu na kunibusu akisema “twende başı baby wangu.”
Nilitabasamu, tukaenda bafuni pamoja. Başı vile haoni, ni kupapasana, kucheza na kucheka. Nilikuwa na furaha sana kusema kweli, nilikuwa nafurahia kupita kiasi kwenye maisha yangu sijawahi kufurahia maisha namna hii. Kumbe kuna kufanya mapenzi na kuna kufanya mapenzi na mtu unaye mpenda.
Nakuambia huu usiku ulikuwa wa vilio na kucheka nakumbuka kuna muda mama Babuu alikuja kugonga. Niliinuka na kwenda kufungua akaniuliza “boss kwema nimesikia kelele nilidhani hampo sawa.”
Nikaingiza kichwa chumbani kumtazama Pina tukacheka pamoja hata mama Babuu alijikuta anacheka akisema “naomba nikalale tu.”
Nilicheka nikisema “usiku mwema mama yangu nakupenda sana.”
Nikarudi Chumbani namwambia Pina “Umeona sasa, hadi watu wanajua tunagombana kumbe ni vile unaniua.”
Alicheka halafu nilisema “tuzo ya usiku wa leo inakuja kwako LOML. Umeshinda, wewe sio wa polepole.”
Alinikumbatia na kusema “baby wangu, nashukuru sana kwa kıla kitu. Kusema kweli Naomba Mungu hii furaha yetu isiishie hapa, furaha yetu idumu siku zote. Nakupenda kuliko kawaida. Nakupenda sana. Nashukuru kWa kumjali mtoto wangu, bibi yangu na maisha yangu yote kwa kawaida. Nakupenda sana.”
Nilimtazama na kusema “huu ni mwanzo tu, bado mpenzi wangu. Subiri tuweke mambo sawa. Nitakufanyia mambo mengi mazuri na ya kupendeza kwasababu wewe ni mpenzi wangu, mpenzi wa maisha yangu na nakupenda.”
Alitabasamu na Akacheka kidogo akisema “umekua unalia kwa huzuni eti aiiiiiii aiiiii babyyyyyy ooohhhhh kama ng’ombe.”
Nilicheka na kusema “niache nilale hapa saizi hata unipe staili gani mama, siwezi kufanya lolote, siwezi kufanya kitu chochote kile. Nitakuangalia tu Labda univamie.”
Tukacheka, basi tulilala tukiwa tumekumbatiana.
Tulilala usingizi mzuri sana, ukiona una shida ya usingizi basi ndugu yangu jitahidi upate mpenzi kama Pina. Na kama ni mdada basi upate kama mimi hapa. Utalala, tena utalala usingizi ambao hutaki kuamka utataka ukae tu hapo na mpenzi wako kitandani. Kusema ukweli, mimi sikuwa hata naumwa nimepona kabisa. Nina hali nzuri sana.
Tulilala, asubuhi niliamka namtazama tu mrembo wangu. Na yeye aliamka na kusema kwa sauti ya usingizi “Morning handsome!!”
Nilitabasamu nikisema “Morning LOML, upo vizuri Beutiful?.”
Alitabasamu na kusema akideka “Najuaje vizuri na sijapata morning kiss babe. Kiss Me.”
Nilitabasamu, na Kisha nilimbusu midomo yake, Akatabasamu na kusema “baby, sasa mswaki hatujanunua.”
Nilisema kWa upole “ipo ya kutosha kabisa.”
Alisema akicheka “No!!, sitaki mwingine, unaonaje tukishare.”
Nilitabasamu tu, alinipa mikono nimsaidie kumuongoza. Nilifanya hivyo na kumchukua mpaka bafuni. Aliniambia “nimechoka wewe hapo ndiyo unipigishe mswaki.”
Nikacheka na kusema “your wish is my command LOML, haya fungua mdomo wako.”
Alifanya kama nilivyosema, nilimsukuma meno, na yeye kwa kupapasa papasa alinisugua hata wakati mwingine ananipaka usoni maana sioni mimi nacheka tu. Baada ya hapo sasa tulioga pamoja, akanitania “vipi sasa asubuhi hufanyi mazoezi?”

