LOML | Love Of My Life (237)

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:237
Baba alinitazama na kusema “mwanangu najua mama yako amekukwaza msamehe si unajua mambo ya wakina mama.”

Mama alinitazama na kusema “mwanangu ni kweli nilikuwa sitaki uachane na Gabby lakini Baada ya kujua lile sitaki kusikia hata. Lakini kusema kweli sijui kwanini huyu kipofu.”

Nilichukia na kusema “baba ongea na mke wako tafadhali. Hakuna kitu sipendi kama anavyo muita mpenzi wangu kipofu. Mama anaitwa Pina, ni mwanamke wangu, atakuwa binti yako. Utake au usitake unanielewa sijui.”

Mama alisema “mume wangu unaona, mtoto amerogwa huyu. Hawezi kunijibu mimi hivyo. Labda niwe nimekufa vinginevyo hawezi kumuoa Yule binti kabisa yani.”

Baba alimtazama mama na kusema “huna aibu, una Salı nini. Mimi ni baba yake na Pina nimempokea ni binti yangu. Kama wewe hutaki mimi nitahakikisha hawa wawili wanakuwa pamoja. Unakuaje na roho mbaya hivyo huna huruma hata kwa mtoto wako.”

Niliona tu watagombana hapa, nilitumia ustaarabu nikamwita mama babuuu, alikuja na alipofika nilimwambia “tafadhali waandalie baba na mama Chai.”
Baba alisema “hapana mwanangu, tushakunywa.”

Nilimtazama na kusema “sawa baba, mimi ndiyo nilikuwa najiandaa niende kazini tutaongozana au kama bado mpo nimwambie awaandalie chakula.”

Baba alisema “sisi tunaondoka mwanangu. Nitakutafuta kuna jambo tuzungumze.”
Nilitabasamu tu kwa uongo na kusema “Sawa baba yangu.”

Mama alinitazama na kusema “mwanangu, najua unakasirika. Sina maana mbaya mwanangu. Simaanishi kitu kimoja. Inanisumbua na nashindwa kabisa kujizuia. Nadhani unanielewa mwanangu. Sijui nitawezaje kukabiliana na hili. Yote kwa yote unajua tupo pamoja na nakutakia mambo mazuri.”

Nilitabasamu na kusema “wewe ni mama yangu. Sijui unawaza nini kichwani Ila mimi najua una niombea Mara zote. Sitakulazimisha umpende Pina. Ninao uhakika kuwa yeye ni mwanamke wa maisha yangu.

Ni mwanamke mzuri kwangu. Nashukuru Mungu kwa hilo na namshukuru Mungu nimeondoka kwa Gabby. Tuanze maisha mapya sasa wazazi wangu. Nawapenda sana na Asanteni kwa kuja.”

Mama alinikumbatia, nilikumbatiana naye na Kisha baba na yeye alinikumbatia na waliniaga. Niliwatazama tu na kutikisa tu kichwa changu maana hi wazazi wangu na wanavyobishana mpaka naona huruma tu maana Wangejua Pina anavyonipa mimi, sina hata habari ya kumuacha. Hapa nataka tu mambo ya taraka yapite kiasi ndiyo nianze kuwaza juu yangu na Pina wangu.

Mama na baba yangu Baada ya wao kuondoka, nilirudi haraka chumbani kwangu. Baada ya kufika chumbani nilikutana na Pina akiwa amekaa tu na hali ya huzuni. Niliita “Pinaaa!!, Pina mpenzi upo sawa?”

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata