LOML | Love Of My Life (241)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️: 241
Nikamuelezea ilivyokuwa, ndipo Willy alisema β€œkuna mabingwa wa macho kibao ndugu yangu. Hapahapa Tz kuna hospitali Zina hawa wabobezi. Subiri nitakupa majibu kwenye hili. Uanzie hapo unaweza kuta hata sio lazima muende mbali huko.”

Nilimtazama na kusema β€œupo sahihi kaka, hapa muujiza unahitajika. Halafu kaka, ukisikia eneo zuri, kiwanja namaanisha kinauzwa mahali. Nilitunza visenti vyangu naona muda umefika.

Siwezi kuishi na Pina kWa nyumba ambayo niliishi na Gabby Tena vibaya. Pina Ana stahili heshima.”
Willy alitabasamu na kusema β€œnapenda unavyo ongea kama mwanaume. Safi sana.”

Nilitabasamu tu, Willy aliendelea β€œupo sahihi. Pina anatakiwa apate kwake pia, Ila Mwambie na baba hawa wazee usiwadharau wana mambo hao hawa.”
Nilicheka tu.

Tuliongea Mengi na mwisho wa siku tuligawana kazi. Hapa nafikiri nikazie tena. Nilikuwa napata kazi mpaka nachanganyikiwa mimi. KazΔ± zilikuwa ni nyingi sana kwa upande wangu. Sio kazi tu kawaida yaani wateja tena kampuni kubwakubwa, serikali, watu binafsi wafanya biashara wakubwa na mahotel. Watu hawa wote walikuwa wanahitaji huduma kwenye kampuni yangu. Hata nakumbuka nilipokuwa nikitingwa hivi sikuwa nasahau kuhusu mpenzi wangu.

Ilifika mpaka ijumaa, nilimpitia Pina nyumbani kwao, tena kwa upendo sana. Tulipata chakula nje na nyumbani. Tukafanya manunuzi ya hapa na pale na kurudi nyumbani. Mama Babuu alitupokea kwa upendo sana. Na tuliingia zetu chumbani.

Huku chumbani ni raha tu kwa kwenda mbele. Huku ni kuserebuka tu. Hata nakumbuka usiku tukiwa tunaongea hili na lile nilimuelezea namna Mungu ana fungua baraka.

Mpenzi wangu aliniambia β€œMpenzi unajua sasa unaweza kufungua ofisi nyingine ndani ya ofisi hiyohiyo.”
Nilimtazama na kusema β€œUnazungumzia nini sasa?”

Alitabasamu na kusema β€œMfano kuuza mataa makubwa ya urembo yale ya ufahari, vitu vizuri vya mapambo si watu wanataka nyumba zao zipendeze kisasa, basi huduma kama hizo yaani unakuwa una mafundi wa finishing na mambo Kama hayo mimi sijui nilitaka kusema nini Ila si umeelewa?”

Nilimtazama na kutabasamu na Kisha nilisema β€œhivi unajua una akili Ila basi tu unajutoaga ufahamu. Ni wazo zuri sana hilo, tena hapo tena naweza fungua na biashara nyingine tena, tupilia mbali mambo ya ujenzi hapa masuala ya mavitu ya kisasa kama tv, fridge, radio, jiko za kisasa unaona eenh yaani mtu akija kwetu anaondoka na vitu muhimu maana vyote tunakuwa navyo. Unaonaje?”

Pina alitabasamu na kusema β€œsasa je?”
Nilitabasamu na kusema β€œuna akili sana wewe, Asante sana sasa hili La ujenzi afanye Willy mimi nitafanya haya mengine ya babe wangu.”

Tulicheka na kufurahia sana.Hakika palipo na wawili na mazungumzo yenye faida mtatoka na kitu. Mimi binafsi kΔ±la maneno ya mwanamke wangu kuhusu kazi au mfanikio nilimsikiliza na kuyafanyia kazΔ± kichwani.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata