LOML | Love Of My Life (243)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️: 243
Baba alinitazama na Kisha alisema β€œmambo mazuri hayataki haraka kijana wangu. Kwasasa tuna mambo mengi kwanza wazo jipya La biashara, mbili ni kuhusu yeye mwenyewe aone tena na ndiyo kitu nilitaka tuzungumze hapa.

Hivi vyote vina hitaji pesa. Sio kwamba kupata nyumba mpya ni vibaya lakini mwanangu hatuwezi tumia pesa zote tukakosa akiba. Kitu najaribu kusema ni kuwa kwasasa tuangalie macho na biashara.

Wakati huo tunatafuta eneo mdogomdogo, tuna akiba ya kutosha si unajua hatujui ya kesho na wakati huo biashara tunatazama inaendaje kama tuongeze hela au tuachane nayo.

Tukiona biashara inarudisha pesa sasa ndiyo tuna rudi kwenye kujenga kitu ambacho hela ikiwepo ni ndani ya miezi tu au mwaka mnapata nyumba yenu nzuri kabisa, nzuri sana na familia mnayotaka.”

Nilitabasamu na kusema β€œUmeongea vyema baba. Hata hivyo sitaki tena sherehe inatosha ndoa ya kwanza. Ndiyo maana wewe ni baba yangu. Naendelea kujifunza kutoka kwako kipenzi baba yangu haya niambie kuhusu macho imekuaje?”

Ndipo baba alinielezea kuwa aliunganishwa na daktari bingwa wa macho na rafiki yake wa karibu. Alianza kuwasiliana na huyo dokta na yeye alimshauri kuwa Pina aanze tu kuhudhuria clinic ili kupata taarifa zake vizuri kabisa kwani kuna wataalamu wa macho kutoka India watakuwa nchini miezi kadhaa ijayo kwaajili ya watu wenye matatizo makubwa ya macho. Hii ni nzuri kwetu haina haja tena ya kwenda mbali au sasa ni sisi tuamue.

Nilitabasamu na kusema β€œmimi naona ni nzuri sana, naona wala haina shida kabisa. Kwasababu mwaka huu tuna mambo Mengi. Tuanze hapa halafu tuwasikilize watasema nini na ndiyo tutafuata wanachosema.”

Baba alikuwa na furaha tu, unajua mazungumzo kama haya huleta raha sana.

Baada ya muda Pina wangu na Fimbo yake alitoka, hakuwa anajua nipo na baba basi anaita β€œBaby, mpenzi wangu Upo wapi?, itika basi, baby!!, loveeee!!, unafanya hivyo kwanini lakini, niitikie mwenzio nakuomba.”
Mimi nacheka, baba anasema β€œsi umuitikie.”

Mimi naona raha vile ananiita hata alisema β€œNisikukamate utalipia mabusu mengimengi.”
Baba alisema β€œooh ishakuwa kazi mwisho atukane mbele yangu acha ujinga.”

Niliona baba yupo sahihi, niliinuka na kumfuata. Akawa anadeka akisema β€œsasa mbona naita huitikii lakini, kwanini unanifanyia hivyo?”

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

BINTI MDUNGUAJI FULL

KIAPO CHA MASIKINI FULL

CHAGUO LA MOYO FULL