LOML | Love Of My Life (250)

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️: 250
Nilicheka na kusema “mama usinifanyie hivyo na usimdanganye binti wa watu. Vannesa kama mama yangu amesema sina mahusiano anakudanganya.

Mama siwezi, sina nguvu za kumuacha Pina mimi. Ninampenda yule mwanamke sio mwingine. Kwahiyo huyu Vannesa wako mtafutie mwanaume mwingine.

Binti Vanessa ulimwengu wa kutafutiana wanaume ulipita. Sasa hivi vijana wenzako wote tunapambana wenyewe.Usimsikilize mama yangu. Anajua kila kitu.”

Binti alimtazama mama, kisha mimi macho yakiwa yanatoa machozi. Mama yangu sasa. Nilishindwa vumilia nikaangua kicheko. Binti aliinuka na nguo yake sasa kavaa anaenda kupelekwa kwa mchumba mpya. Nilimtazama na alivyo jipamba mimi sina mbavu.

Aliinuka kWa hasira akiondoka , mama aliita “Vannesa!!”
Mimi Nilicheka nikisema “mama mfuate tu amechukia sana anaweza kuanguka kwa presha. “

Mama aliinuka na kusema “Ricky, ulichokifanya leo sitakusamehe. Umenivua nguo, umenikosea sana na upo hapa unacheka. Huyo mwanamke wako, na wewe mwenyewe mtaona kama mtafunga hii ndoa bila baraka zangu.”

Nilicheka na kusema “mama unanikera sana unajua. Baba anatosha hata wewe usipotaka. Mimi kumuoa Pina hata niwe wapi ni lazima, ni lazima kabisa wewe kahangaike na Vannesa.”

Mama alinitazama kwa hasira sana na alitoka kumfuata mgeni wake, nilibaki nacheka na wakati huo mama Babuu na yeye hana mbavu. Nilicheka nikisema “Mama Ricky ana vituko sana Leo kaniletea mchumba kabisa. Nikimwambia baba atacheka sana.”

Niliinuka kuelekea chumbani nikiwa mwenye furaha kubwa sana. Nacheka Sina mbavu hata nilimpigia baba namsimulia huku nacheka sana. Nilikuwa nacheka naona mama anavuka mipaka yake.

Upande wa baba alikasirika sana hata alisema “Naona mama yako anachanganyikiwa sana, mi kitu gani anafanya leo lazima niongee naye anielewe kwanini anakuwa mjinga namna hii.”
Mimi nacheka, baba anasema “unacheka unafikiri mama yako ana akili nzuri?”

Nilisema nikicheka “natamani ungekuwepo baba, yaani mama nashindwa kabisa kumuelewa.”
Baba alikata simu. Nilibaki tu namtafakari mama yangu na sipati majibu kabisa.

Maisha yaliendelea mama na mume wake sijui ilikuaje huko nyumbani. Ila mimi na Pina kila siku kama sherehe na muda mwingi tunakuwa pamoja.

Tuliendelea na maisha na tangu niachane na Gabby ilikuwa ni Kama Miezi 9 hivi wakati huo nyumba yangu ipo hatua za mwisho sana. Siku hii nilikuwa ofisini, alikuja Willy ananitazama anacheka hata nikamuuliza “Vipi ndugu yangu?”

Aliniambia akitabasamu “ndugu yangu una nyota sana. Unapata wanawake wacha Mungu sana. Hizo comments sasa.”
Nikamwambia kWa upole “ni nani tena ongea nikuelewe.”
Akatoa simu na kunipatia.

Alikuwa ni Gabby eti anajiita Jesus daughter. Nilitamani kucheka, nikasema “Willy emu acha ujinga kwa mtoto wa watu. Pengine anabadilika kweli ingawa mimi simuamini kabisa.”

Willy anacheka anasema “Soma Comments.”
Başı nikafungua hiyo post Willy kanionesha alikuwa anaimba gospel hata analia.

Mimi ninasoma comments eti wanamwambia “mkiachwa ndiyo Mungu, Mara ooh baada ya Muacho, wengine huyu si ndiyo mume wangu this mume wangu that, wengine miss Dadie, wengine wanamuuliza Bedo yuko wapi, mwingine sijui ana mfahamu Aliandika acha usagaji kwanza.”

Comments ni mbaya za kuumiza , naona mtandaoni ndiyo panamtesa zaidi Bora angeacha.

Nilimtazama Willy na kisha nilimpa simu na kusema “Willy kaka, Mathayo 7:1 “Usihukumu ili usije ukahukumiwa. Anajua yeye na Mungu wake. Wapo watu wengi kwenye haya maisha wakabadilika na kuwa watu wazuri sana. Yeye ndiyo anajua ndani ya moyo wake kitu gani anafanya.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata