LOML | Love Of My Life (251)

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️: 251
Tusiwakatishe tamaa wale wanao jaribu kubadilika kwenye maisha yao. Najua kuwa maumivu yanatufanya tusiwaamini. Lakini tujitahidi tusiwe sehemu yao ya kuanguka, tusiwaingilie kabisa, tuwaache watafute amani yao ili kama wakiwa wanaanguka tusibebe dhambi zao.

Kaka sitamani kujua habari za huyu mwanamke hata kidogo, na kamwe siwezi kumuamini kwenye maisha yangu. Muache tu aishi maisha yake.”

Willy alinitazama na kusema “kaka kweli umeamua, na nimekuelewa. Kwakweli Kama hatuwezi kuwaunga mkono baada ya kutuumiza basi tusiwe sababu ya kuwakatisha tamaa. Wajipambanie wenyewe.”
Nilimtazama na kumuuliza “eenh vipi kazi?”
Alinipa report zake za hapa na pale. Mimi nilikuwa tu nafanya haya sitaki kumuona wala kusikia kuhusu Gabby.

Nikiwa hapa nazungumza na Willy simu yangu iliita. Alikuwa ni Dokta wa Pina.

Nilipokea na Dokta alisema “hongereni na pole sana kwa kusubiri. Tumefanya mazungumzo na wabobezi walisema wanakuja na sasa imefika mwisho.

Wiki hii jumamosi watakuwa hapa. Hivyo kWa heshima yako, Tunaomba mjiandae na mfike hapa mapema sana siku hiyo kwaajili ya vipimo na matibabu. Tunawatakia kila jema.”

Nilitabasamu na kusema “Asante sana Dokta, Asante sana.”
Nilikata simu, na Willy aliniuliza “kuna nini, mbona una furaha namna hii?”

Nilimtazama na kusema “mwezi huu Pina anaweza kuona. Naogopa sana hivi si anaweza akanikataa mimi baada ya kupona, Labda mimi sio aina ya mwanaume anamtaka, sijui itakuaje naogopa. “

Rafiki yangu alicheka na kusema “ni mwanamke Gani akatae mwanaume mwenye roho nzuri kama wewe. Furahia tu sasa mtachat vizuri kabisa, mtaonana vizuri kabisa Mungu amsaidie anaonekana ana imani sana ataona.”

Nilitabasamu na kusema “nataka nimvalishe pete ya kuomba Uchumba jumamosi ili tutibiwe akiwa mchumba wangu. Kisha akisha Pona nimuoe akiwa anaweza kuniona vizuri.”

Willy alitabasamu na kusema “wachaaa weeee, sijui hata itakuaje.”
Nilicheka na kusema “wacha nimpigie kwanza halafu Baada ya hapa tutapanga.”

Nilichukua simu na kuanza kumpigia Pina. Pina alichelewa kupokea simu, nilikuwa na furaha sana unajua. Başı alipopokea nilisema kwa furaha “Love of my life. “
Aliniitikia “Yes baby, upo vizuri?”
Nilishtuka na kusema “hauna furaha kwasababu gani?”

Alishusha pumzi na kusema “no baby, nimechoka sana. Niambie kuna nini ni Kama umefurahi sana.”
Nilitabasamu na kusema “ni kweli mpenzi, dokta wako amenipigia.”
Akaniambia “eneh Kuna nini?”

Nikamuelezea, Pina alifurahi sana na kusema “waooo Mungu mwema jamani, nina hamu kubwa ya kukuona.”
Nilimuuliza “Pina itakuaje kama utaona halafu usinipende?”

Pina alisema “ukiniambia hivyo natamani kukupiga, usiniambie hayo kabisa. Nataka kumuona huyu kaka mwenye roho nzuri kama wewe. “
Nilifurahi na kusema “unasema Kweli Pina?”

Alifurahi akisema “sana naona jumamosi haifiki.”
Nilivuta pumzi na kusema “Kabla ya kufanyiwa upasuaji, natamani nikufanyie kitu Ijumaa kisha Jumamosi nikupeleke hospitali.”

Akaniuliza kWa haraka “kitu gani hiko?”
Nilisema “hapana Subiri tena hapa furaha ni kuwa nina kazi nyingi sana hata hatutaonana mpaka alhamis au ijumaa yenyewe au kama unataka ukakae nyumbani tu lakini nitakuwa busy sana.”

Alicheka akisema “haiwezekani nitakuja Ila na mimi kuna kitu nataka tuongee ijumaa kabla ya huo upasuaji. Nilitaka nikija ndiyo tuongee Ila wacha tuunganishe matukio.”

nikamuuliza “ni kitu gani Tena? “
Alicheka na kusema “hapana Subiri, ijumaa sio mbali.”
Tulicheka tu Ila Kiukweli sauti yake ni Kama ilikuwa tofauti lakini ningesema nini mimi.

Nilikata simu na Willy aliniuliza “vipi mbona hiyo Sura?”
Nilisema kWa upole “sauti yake haipo sawa naogopa kumpoteza.”

Alicheka na kusema “kwanini unakuwa unawaza hivyo hujiamini kabisa.”
Nilisema kWa upole “hujui tu huyu mwanamke akiwa tofauti mpaka roho inaniuma. Atakuwa sawa lakini.”

Willy alisema “watoto wakike wana mambo Mengi sana. Mpe muda atakaa sawa kabisa kwasasa tuwaze Ijumaa. Kwahiyo unafanya sherehe.”

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata