LOML | Love Of My Life (253)

 

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️: 253
Mama alimsukuma Pina, akarudi kuchukua nguo, akatupa nje. Kwenye maisha yangu yote sijawahi kuwa na hasira kama hii siku.

Nilichukia sana, willy sikuweza kumuaga , niliondoa gari huku nalia natetemeka, mama yangu aombe Mungu nisimkute nyumbani. Nilifika nyumbani naita Pinaaaa!!, Pinaaaa!!, Pina mpenzi wangu, Pinaaaaa!!”

Mama Babuu analia anasema “nisamehe boss sikuwa na La kufanya.”
Naita “mamaaa, mamaaaa!!”
Mama babuuu aliniambia “mama ameondoka hapa muda uleule na amesema Pina asirudi hapa.”

Sikutaka hata aendelee, niliingia kwa gari yangu safari nyumbani. Naendesha gari kama mashindano. Nilipofika nilipitiliza ndani naitaaa “mamaaaa!!, mamaaaaaa!!, mamaaaa upo wapiiii!!”

Baba yangu alikuwa ndiyo anajiandaa aliponiona alishtuka na kuuliza “kuna nini, unalia na hasira sana.”

Nililia nikisema “!baba nataka mama aniambie mimi ni mtoto wake au ni Nani yake.”
Baba alinitazama na kusema “wewe ni mtoto wake kwani kuna nini?”

Nilitoa simu yangu na kumpa baba aone mama alichofanya. Baba yangu alichoka na kukaa, mimi nalia natetemeka. Baba aliniuliza “Binti yangu yupo wapi?”
Nilitokwa machozi nikisema “sijui baba, mimi sijuii, sijui atakuwa wapi.”

Baba alinitazama “binti wa watu achana na huyu mama yako kichaa kabisa anatuharibia siku, twende tukamtafute.”

Nililia nikisema “baba itakuaje akipatwa na tatizo, sitamsamehe mama mimi sitamsamehe kabisa.”

Baba alinikumbatia, nilimwambia baba nikifuta machozi “nenda kanisani kule nilifunga ndoa na mimi naenda kwao ukimuona utaniambia nikimuona nitakuambia.”

Baba yangu alisema “sawa mwanangu, kuwa makini usije kufanya ujinga. Huyu mwanamke mpumbavu sana.”

Niliingia kwa gari, niliendesha nalia, nimefika kule nakuta bibi anajiandaa. Nilipomuona aliniuliza “mbona unalia?, kuna tatizo.”
Nilimtazama na kumuuliza “bibi Pina amekuja hapa?”

Bibi alinitazama na kusema “Hapana, sijamuona hapa. Ulikuwa naye, yupo wapi?”
Nililia nikisema “Mungu wangu mke wangu, Mungu wangu.”

Bibi akauliza “nini kimetokea, nililia nikisema “amekwazana na mama yangu, sijui kaenda wapi?”
Bibi alisema “nilijua tu nilijua hili litatokea haya kanisani je. “

Kabla sijajibu simu yangu iliita alikuwa ni baba yangu, baba alisema “hayupo mwanangu vipi huko.”
Nililia nikisema “baba nitafanyaje sasa, nitampata wapi.”

Hali ilikuwa mbaya sana, bibi alichukua simu yake alipiga simu ya Pina inaita haipokelewi, nikapiga na mimi hakuwa anapokea. Bibi alisema “sijui hata atakuwa ameenda wapi, nachanganyikiwa mimi, Mungu wangu.”

Nilisema “bibi mimi naondoka Labda kanifata ofisini kama hayupo huko naenda kanisani nitasubiri mpaka aje.”
Bibi alikuwa ananitazama analia tu, mimi niliingia ndani ya gari nalia sana.

Nilikuwa sielewi kitu zaidi ya kukimbizana gari yangu. Nilikuwa nimekaribia kabisa ofisini kwangu na kwa b

 

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata