LOML | Love Of My Life (254)

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:254
Nilikuwa sielewi kitu zaidi ya kukimbizana gari yangu. Nilikuwa nimekaribia kabisa ofisini kwangu na kwa bahati mbaya kwa kukosa umakini nilipata ajali mbaya sana, ajali mbaya.

Nilikuwa nalia namtaja Pina tu kwa sauti ya maumivu na kukata tamaa “Pina wanguu!!, Pinaaaa!!, nitafutieni Pina!!”

Nilikimbizwa hospitali, taarifa zilisambaa sana. Mpaka nafika hospitali jina pekee nataja ni Pina tu hata sijui alipokuwa. Nilianza kufanyiwa matibabu, Pina simuoni mimi, nalia tu.

Habari zangu zilisambaa haraka. Niliona baba yangu akija mbio kwenye chumba nilikuwepo. Baba alilia akisema “mwanangu nilikuambia uwe makini unaona sasa eneh!!”

Mimi nilimtazama baba na kusema “Pina baba, Pina!!! “
Baba yangu alichanganyikiwa sana, niliona baba yangu anavyo hangaika Mara willy alifika na mama yangu pia.

Nilipomuona mama yangu ni Kama kichaa kilinipanda nikimfukuza na kusema “yote ni kwasababu yako, nakuchukia mama ondoka hapa, ondokaaaa, ondoka.”
Mama analia akisema “nakupenda mwanangu, nisamehe mama yako, nisamehe.”

Nilimwambia baba yangu “baba Naomba mtoe mke wako hapa, na akamtafute Pina popote alipo aje naye hapa.”
Willy alinitazama na kusema “Pina yupo na mke wangu, wanakuja.”
Mama alidakia “wapi niwafuate?”

Nilisema kWa uchungu nikilia “sitaki hata kukuona sitaki!!!”
Nilikuwa na maumivu makali nalia huku mama akilia haamini alicho sababisha huku akisema “mwanangu usifanye hivyo, tulia mwanangu. Dokta aliona mambo magumu sana kwangu, Nilichomwa sindano na kujikuta ninalala.

Nililala muda mrefu sana, kusema kweli nilikuwa na maumivu makali sana. Hata sijui namna ya kuyaelezea ingawa nilikuwa nikitazamwa kwa nje ni kama sijaumia. Nilifumbua macho yangu, niliona Pina amelala Pembeni yangu. Niliita kWa uchungu na maumivu “Pinaaa!!, Pinaaa!!”

Pina haraka aliamka na kuanza nipapasa akisema “Mpenzi wangu, umeamka, umeamka kipenzi.”

Nilikuwa na maumivu siwezi hata kujigeuza, nilisema nikilia “nisamehe sana kwa alicho fanya mama yangu. Nimekutafuta sana Jana, naona aibu kwa kile amekifanya. Nisamehe kwaajili yake.”
Pina alilia akisema “usiongee mpenzi, niambie umeumia sana, niambie mimi sioni niambie.”

Nilimshika uso wake nikisema “Kabla sijakuona nilikuwa na maumivu makali sana yanapoa sasa baada ya kujua ipi hapa na mimi. Huniachi si ndiyo?”
Pina huku ananipapasa alisema “kamwe siwezi, Kamwe. Nakupenda sana.”

Tulikumbatiana, ingawa nilikuwa na maumivu sikuwa najali kabisa. Baba alikuja na Mara niliona mama yangu na akiingia. Baba Alinifuata nilipo, nilimtazama baba na kusema “baba Naomba umtoe mama hapa, sitaki kumuona mimi.”

Mama alipiga magoti akisema “Naomba mnisamehe sana wanangu, nilikuwa mjinga, nilikuwa na hofu, nakupenda sana mwanangu nilitamani vitu ambayo sikutumia akili. Naomba mnisamehe sana.”

Baba alifoka akisema “kelele, keleleeee, mwanamke mpumbavu sana wewe sijapata kuona. Nyakati zote unaniona mimi kama mpuuzi . Kwanini unakuwa na roho mbaya namna hii.”

Mama alizidi kulia kwa uchungu Ndipo daktari aliingia, alipoingia baba alikaa kwa kochi akiwa na hasira, dokta alinitazama na kuniuliza namna naendelea wakati wote huo Pina analia tu.

Nami nikamuelezea. Dokta alisema majibu yangu yapo tayari Nani nimpatie. Baba alisema “mimi ni baba yake, na huyu ni mama yake, huyo ni mke wake. Tupatie tu.”

Dokta alitutazama na kuelezea hali yangu, mwisho wa yote alisema “ameumia sana ndani kwa ndani na hii imepelekea matatizo hata kwenye mirija yake ya uzazi. Asilimia za kupata mtoto ni 10/90Ni muujiza unahitajika. Poleni sana.”

Nilifumba macho yangu na kusema “nooooo!!, noooo!! Unataka kusema sina uwezo wa kuzaa Tena?”
Dokta alisema “uwezekano uliopo hautoshi kusema uwezo inawezekana. Pole sana Kaka.”

Nililia kWa uchungu, nikisema “mamaaaa, ni wewe umesababisha, ni wewe na roho yako mbaya, ni wewe mama, nakuchukia sana , sitaitwa baba kwasababu yako, sitakuwa na familia ya ndoto zangu kwasababu yako. Nakuchukia.”

Pina alilia kwa uchungu na kunikumbatia akisema “Tulia mpenzi, tulia. Utaitwa baba, tulia utaitwa baba.”
Nilimtazama Pina nikisema “kivipi Pina?, nitaitwa vipi baba!!”

Baba yangu alifoka akisema “nakuchukia sana mke wangu, wewe una roho mbaya. Ina maana unataka mtoto wangu na yeye aishi maisha kama yangu. Uliniletea mimba sio yangu na nilipokea mtoto bila kulalamika ukaniona mpumbavu na sasa unataka mwanangu wa pekee, na yeye afanye Kama mimi si ndiyo, si ndiyo?”

Nilishangaa, ninatamani kuinuka lakini siwezi, dokta ananituliza tu, na kısha niliuliza “baba unasemaje, unataka kusema wewe sio baba yangu wa kunizaa?”
Nilijikuta nakumbuka ushauri wake, vile anasema kitanda hakizai haramu, Mara kuwa baba sio lazima uzae.

Baba yangu anavyo nipenda kuliko hata mama aliyenizaa alipiga magoti na kulia kwa uchungu akisema “nisamehe mwanangu, nisamehe sana nilitegemea kwako nitapata wajukuu watakuwa watoto wangu pia, tazama mama yako alichofanya.”

Nilimtazama mama nikilia kwa uchungu nikisema “mamaaa!!, mamaaaa!!, wewe ni mama wa aina Gani!!, ilikuwaje Mungu akakupa wewe uzazi Mungu wangu haufai.”

Pina alinitazama na kusema “tafadhali usiseme hivyo. Wewe utakuwa baba, hivi karibuni utaitwa baba. Mimi nina mimba, miezi miwili sasa. Ndiyo nilitaka nikuambie jana.”

baba yangu alisimama na kusema kwa kushangaa “unasemaje Pina Una mimba mwanangu.”
Nilijikuta nacheka nikisema “una mimba kweli Pina!!, nitakuwa baba, Ina maana nitakuwa. Baba!!”

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata