
LOML | Love Of My Life (255)

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️: 255
Alinijibu akilia “ndiyo utakuwa baba, utakuwa baba mpenzi wangu tulia tafadhali.”
Nilijikuta nacheka huku dokta akipiga makofi na kusema “dokta mzigo wangu, mzigo wangu dokta.”
Hapo mama yangu kapiga magoti chini hata aibu. Dokta alikuwa na furaha sana. Wakati huo bibi na Sam wanaingia. Şam alinikimbilia akisema “baba!!, baaabaaa!!.”
Alinikumbatia akilia akaniuliza “unaumia sana, nilisikia umeumia nimelia sana. pole baba.”
Nililia kWa furaha nikisema “nipo hapa mwanangu, ninaendelea vizuri kabisa nipo hapa.”
Baba alikuwa anashangaa tu, alikuja nikumbatia kwa furaha kisha na Pina alikuja. Dokta alinipa pete yangu na mimi nilisema “Pina ilikuwa kwaajili ya Jana, Kabla hujaenda kwenye upasuaji tafadhali, utakubali kuwa mke wangu?”
Pia alilia kwa furaha akisema “nipo tayari Ricky, nakupenda sana. Nilikuwa naogopa nilijua hadithi mbaya itajurudia.”
Nilimvalisha Pete Pina wote tukilia, mama aliendelea kulia mpaka kwa Pina. Alishika miguu ya Pina na kusema “nisamehe mwanangu, naona aibuuu nakuomba nisamehe sana binti yangu.”
Pina alisema “usijali mama, nipo hapa kwasababu ya Ricky na Hakuna kitu kitabadilika mimi ni yuleyule mshamba na maskini, sijabadilika.”
Mama alilia akisema “tafadhali mwanangu nakuomba.”
Pina alikuwa amenikumbatia tu, hataki msikiliza mama yangu. Simu ya baba iliita, na ilikuwa imetoka hospitali kwa Pina. Baba alinitazama na kusema “Pina anajitajika wamekutafuta sana bila mafanikio.”
Pina alinitazama na kusema “Naogopa sana, tafadhali mpenzi.”
Nilisema kWa kumtia moyo “fanya kwaajili yangu na mimi napambana kwaajili yako hapa. Utakuwa na baba mimi hapa nina willy, bibi na Sam.”
Mama alisema “Mungu akusimamie mwanangu, nenda usiogope.”
Hakuna hata aliyemjibu.
Baba alimkumbatia Şam akisema “mlinde baba mimi nampeleka mama hospitali.”
Şam aliitikia tu. Pina aliagana na bibi yake, akanibusu akisema “Asante sana mpenzi nitarudi hapa mzima.”
Nilimwambia nikitabasamu “kuwa makini, mwanangu na wewe mrudi sana.”
Şam aliniuliza “mwanako mwingine?”
Wote tulijikuta tunacheka.
Nilipokea habari mbaya kuwa nimeharibikiwa na mfumo wangu wa uzazi lakini Kumbe tayari Pina ana mimba yangu kwangu ilikuwa habari njema hata ndani ya moyo wangu Naomba Mungu anipe mapacha.
Nilikuwa nasema “Mungu unajua napenda familia, napenda watoto tafadhal sijui utafanya nini Ila nina imani nitakuwa na familia kubwa sana.”
Nikiwa katika Hali hii mama alinifuata na kunipigia magoti akisema “mwanangu mimi ni mama mbaya kwako. Nilijali furaha tu kuliko unajisikiaje. Najutia sana mwanangu. Sikujua nitasababisha matatizo hivi. Tafadhali mwanangu Naomba nisamehe sana. Naomba nisamehe sana mwanangu.”
Nilimtazama mama na kusema “mama nahitaji pumzika, umemkosea Pina. Akikusamehe nitakusamehe pia. Naomba niache mama.”
Mama alilia sana hata bibi Pina alimuinua na kutoka naye hapa.
Siku zote nilikuwa siongei na mama nimenyamaza tu. Walikuja watu mbalimbali kuniona wakiwepo mama Gabby na baba Gabby. Baba alimuulizia Gabby.
Nilisikia mama Gabby alisema “Mungu ndiyo anajua, mwanangu kama kichaa anavuta sigara, pombe, sijui hata kama hatumii madawa.”
Nilisema “niliona amebadilika lakini!!”
Mama Gabby alisema akilia “ni makosa yangu. Nilimdekeza mwanangu Kama yai. Ukiachana na aliyojifunza kwangu Kama mama lakini dunia nayo imemfundisha mengi zaidi.
Natamani wazazi wawachunge sana watoto, wasiwape simu wakiwa wadogo wanaona vingi sana ukichanganya na malezi ya nyumbani ndiyo kabisa. Sijui hata nitafanya nini, nimepoteza.”
Nilimwambia “pole sana mama, poleni.”
Alisema kWa upole “nashukuru na Hongera nimesikia unatarajia mtoto na umechumbia.”
Nilitabasamu tu na kusema “nashukuru sana mama.”
Başı waliaga huku mimi moyoni nikishangaa namna habari zinaenda haraka sana.
Niliwahurumia sana Ila nitafanya nini maisha ndiyo nisha yaanza upya. Kıla baba akirudi namuuliza kuhusu Pina, baba alinipa taarifa zote muhimu, akinisisitiza nisichoke kuomba.

