
LOML | Love Of My Life (256)

𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️: 256
Siku ya pili nilipokea taarifa upasuaji umefanikiwa sasa ni kusubiri matokeo. Nilikuwa namuombea sana mke wangu pale kwenye vitanda vya hospitali.
Na siku zilizidi kwenda na mimi walau nikipata nafuu, wiki mbili baadaye baba alinipigia simu na kusema “mkeo amesema hataki kufunguliwa macho yake mpaka uwepo ili kama amefanikwia uwe wa kwanza kwake. “
Nilitabasamu kwa furaha, niliomba ruhusa hapa hospitali niende kwa mke wangu. Nilipewa ruhusa niliondoka na Mama, bibi, Şam na Willy na mke wake. Baada ya kufika hospital aliyokuwa mke wangu, nilifuata utaratibu na kuingia kwa chumba cha mke wangu. Nilimsalimia kwa furaha. Nilimshika mkono na walimfungua taratibu. Huku tukisubiri aseme kama anaona.
Mke wangu alianza nipapasa uso wangu, huku nikimuuliza “unaniona, unaniona!!”
Mke wangu machozi yalimtoka na kutikisa kichwa kuwa hanioni. Nilitokwa na machozi ya huzuni nikisema “usijali mke wangu, wewe bado ni mzuri. Huu ndiyo Mpango wa Mungu. Mimi bado nakupenda na nitakuwa Ricky yuleyule siku zote.”
Mke wangu kwa furaha ya machozi alisema “you are so handsome Ricky, unafanana na roho yako. Tazama ulivyo. Macho yako, mdomo wako, pua yako, ngozi ooh Mungu wangu Nakupenda sana.”
Nilijikuta nacheka na kumuuliza “unaniona?”
Alitabasamu na kusema “naona, naonaaaa!!”
Nilianza kucheka nikisema kwa vidole “hii ngapi?”
Anajibu “nne.”
“Hii ngapi?” Nauliza na yeye anajibu.
Nilikuwa nasukumwa kwa kiti mwendo nilijikuta nimesimama na kumkumbatia na kutoka nje nikisema “ameonaaaaaaa, ameonaaa!!, Mke wangu anaona!!”
Watu walifurahia wote tuliingia ndani. Başı mtu akiongea yeye anasema ni Nani, alipofika kwa Şam wake walikumbatiana kwa furaha sanaaaa Mara ya mwisho alimuona akiwa na umri mdogo sana.
Alimkumbatia bibi yake kWa machozi na kisha baba yangu akilia na kusema “nilizika wazazi zamani sana kwako nahisi nimepata baba.”
Alifurahi sana baba na kusema “wewe ni binti yangu kipenzi na nakupenda sana.”
Başı kWa Willy, alimtania na wakajikuta wanacheka, mpaka kwa mke wa Willy kisha kwangu akisema “Nakupenda sana Ricky wangu, Nakupenda.”
Tulikumbatiana, mama alitufuata na kupiga magoti, kisha alilia kwa uchungu pale chini.
Pina alimuinua mama na kusema “wewe ni mama nakuelewa, ulipambania kilicho Bora kwa mwanao ingawa kwa njia mbaya. Mimi binafsi nimekusamehe na sikumbuki tena mama.”
Mama alilia akiniita “mwanangu!!, mwanangu!!”
Başı tulikumbatiana pale kwa furaha sana.
Tukiwa na furaha basi kaka mmoja aliita kwa heshima “Dokta Pina tafadhali unaweza kurudi kuketi?”
Baba alishangaa akisema “dokta Pina?”
Başı yule kaka alisema “ndiyo nilifanya naye kazi hospitali Fulani hivi ya Private miaka ya nyuma kidogo. Mimi nilikuwa nesi pale. Kwahiyo huyu ni dada yangu kazini tena boss kabisa.”
Nilicheka na kisha nilisema “ni kweli, changamoto za maisha zilikatisha ndoto zake.”
Baba alisema “haiwezekani, pona kwanza tutaongea kuhusu hili.”
Tulicheka sana.
Na mama alisema “ama kwa hakika usimdharau usiye mjua. Unaweza kuta yupo hapo kwasababu ya maumivu na wewe una mzidishia maumivu kwa kumdharau. Nisamehe binti yangu.”
Pina alitabasamu tu.
Pina alikuwa anabaki hospitali kwa kumchunguza zaidi na mimi nikarudi hospitali. Baada ya Muda Pina alitoka na hakuwa anatumia vitu vyenye mwanga kama simu, tv, kusoma na vitu Kama hivyo. Lakini muda wote alikuwa na mimi pale hospitali akinitazama na mimi nikiyasifia macho yake yalivyo mazuri. sikuwa naamini kabisa, basi ananisimulia namna mama Babuu alivyoshangaa tunacheka na mambo Kama haya.

