LOML | Love Of My Life (258)

๐‹๐Ž๐Œ๐‹ (๐‘ณ๐’๐’—๐’† ๐’๐’‡ ๐’Ž๐’š ๐’๐’Š๐’‡๐’†) โฃ๏ธ: 258
Mimi na Loml miaka 15 ya ndoa yetu nilimpeleka Paris. Alifurahia sana na kutamani kupiga picha kila mahali. Anaona sasa ingawa anatumia miwani Ila anaona na tuna watoto wazuri sana. Kusema kweli kwenye biashara mke wangu kanizidi maarifa na akisema fanya ukifanya unafanikiwa, na akisema usifanye baลŸฤฑ usifanye.

Baba yangu niliyejua ni baba yangu sio baba yangu mzazi na amenilea siku zote kama baba mzazi na hili linatosha kwangu upendo wangu Upo palepale na yeye ananipenda kuliko kawaida na ndiyo upendo nampa ลžam.Usikate tamaaa kwasababu umezaa huyo mtoto ni baraka yako na siku Utakutana na love of your life atampenda huyo mtoto na Hakuna mtu ataamini sio wake kama mimi na ลžam wangu.

Sijawahi sikia mke wangu kuhusu baba ลžam sisi tunaishi maisha yetu na mke wangu ndiyo mke niliyemtaka maishani. LOVE OF MY LIFEโฃ๏ธ (LOML).

Willy ni ndugu sasa, familia zetu zimeungana na tunasaidiana kwenye mambo mbalimbali ya maisha yetu na maisha yetu yanasonga mbele kila siku.

Kwenye maisha yako siku zote kumbuka haya maneno Unatakiwa kujua kuwa sio kila mtu kwenye maisha yako anapokosea anatakiwa kupata nafasi nyingine ya kuendelea kukukosea kwasababu kiuhalisia ni kuwa watu wanapokosea wanajua kuwa wanakosea Ila wameamua kuchagua kukosea.

Mara nyingi watu wanakuona una maana kama tu una faida yoyote kwao.Na unapokuwa kwenye nyakati ngumu kama hฤฑzฤฑ Hakuna mtu wa kukusaidia, kujisaidia ni jukumu lako wewe mwenyewe sasa uchague kuzama au kuwa mshindi.

Hakuna mtu wa kukuvusha mpaka ufungue moyo wako wewe mwenyewe kwasababu muda hauponyi kila kitu badala yake unaficha tu maumivu yako lakini baadaye utayakumbuka tena na Utalia ikibidi ili uwe sawa.

Kikawaida watu wanakutendea kulingana na unavyo Vumilia, ukivumilia leo kesho anaongeza anajua una uwezo wa kuvumilia.

Maisha yetu haya sisi wote tunavaa vinyago, ni vile tu wengine tunavaa vizuri tusionekane upande wa pili na wengine wanavaa vinyago sio vyao ndiyo wanaonekana wabaya mbele za watu haina maana wengine hawana upande wa pili.

Hata kama upo na kila kitu, kama huna ujasiri utadharaulika tu.Wema Bila mipaka, hukaribisha dharau kubwa sana. Ukiendekeza wema utakuwa unakosea kila siku kwasababu watakuumiza tu.

Hata siku moja mapenzi hayabadilishi mtu Bali maumivu, maumivu ndiyo hufanya tujue uwezo wa mtu kitabia.Kamwe huwezi mfurahisha mtu ambaye kwake furaha ina tafsiri tofauti hata yeye mwenyewe hajifurahii.

Wapi watu wanaomba msamaha ili tu waendelee kukuumiza ndiyo wanapenda hivyo.Amani ni gharama sana, Ina chukua akili, moyo, watu wako, na sadaka ya vingi kupatikana.

Gereza pekee gรผmรผ kulikimbia ni maumivu, maumivu, sio kila Vita ni za kupigana, zingine ni kuweka mipaka tu inatosha. Utahangaika sana Ila mtu anaweza tafuta mbadala wako kwa sekunde tu.

Kitu pekee unaweza kufanya sasa hivi, ni kujisahaulisha kila kitu kwasababu Mipaka yako itawaudhi wote waliozoea kukutumia ovyo. Nakuambia hivi kwasababu nimewahi kuwa kwenye hali kama hii, hali ya maumivu sana.

Kwenye maisha yako Hakuna kitu kinaitwa bahati mbaya. Kฤฑla kitu kinachotokea kฤฑna sababu zake. Muhimu Kumbuka kwenye maisha yako kumuita Mungu, kwenye raha zako Kumuita Mungu. Na Siri kubwa ni kumshukuru Mungu kwa kila jambo na kutolea sadaka kila chako, watoto, biashara, mume, mke , familia vyote vinahitaji sadaka na maombi.

Ukiwa unasali mshukuru Mungu kwa kusema โ€œMungu baba yangu wa Mbinguni, umenibariki kwa namna nyingi sana na nakushukuru sana.Ninatambua mipango yako juu ya maisha yangu ni mikubwa na inapita uelewa wangu.Na siwezi kuifikia kwa vyovyote.

Naomba uniongoze na uzidishe imani yangu kwako baba yangu.Ninaweka maisha yangu, ฤฐmani yangu, kazi yangu, mke wangu, mume wangu, mama yangu, baba yangu, mtoto wangu, familia yangu kila kitu changu na kesho yangu nisiyo ijua mikononi mwako.

Ulinivusha na Yale, ninakuamini sana kwenye haya, nina imani na wewe bila wasiwasi wala kusita.Ongoza maisha yangu na wote walio nizunguka.Haswa wale ninaocheka nao kumbe ni adui zangu wakiwa sirini Nipe macho niwaone na niepukane nao.

Adui zangu wasiniweze wala kunisogelea, nifanye wapekee na vile unavyotaka. Watu wakiniona mimi wakuone wewe Mungu wangu. Wewe ni kimbilio langu siku zote za maisha yangu.

Kitu pekee sijutii kwenye maisha yangu ni kukufahamu wewe, Nakupenda sana Mungu wangu wa mbinguni.Nakupenda.โ€

Kwenye maisha kila siku utaona mapenzi mabaya mpaka pale ukutane na mtu ambaye mnaongea lugha moja, mnasikilizana, mnaelewana, mnaoneana huruma na wengi huwaacha watu hawa kwasababu ya mahitaji yao na kwenda kukaa kwenye mahusiano na mwanaume ambaye ana mwanamke wake mahali au mwanamke ambaye ana mwanaume wake mahali na kuishia kusumbuana kila uchwao.

Ukiwa na tabia mbaya ukipata nafasi ya kubadilika badilika na usitafute sababu kwasababu Mtu aliyezaliwa na Mungu haendelei na tabia ya kutenda dhambi, kwa maana ana asili ya Mungu; hawezi kuendelea kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa na Mungu.

Mimi na familia yangu tunasali pamoja, tunafunga pamoja na tuna mwamini MUNGU. Mke wangu aliamini atapona na kuona ikawa na mimi niliamini nitakuwa na familia kubwa imekua. Muamini Mungu tu.

Sio kila mara unapomwona mchezaji anaingia uwanjani anaingia uwanjani kwa ajili ya mechi au mashindano. Mchezaji anaingia uwanjani mara nyingi zaidi kwa ajili ya maandalizi na mazoezi kuliko anavyoingia kwa ajili ya mechi au mashindano.

Kiwango cha ufanisi cha mchezaji katika mechi au mashindano kinategemea sana alijiandaaje na mazoezi aliyoyafanya. Kuna mazoezi anayoyafanya mchezaji ambayo yanamwongezea nguvu. Yapo ambayo yanamwongezea pumzi.

ย 

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

SIMULIZI YA INGIZA FULL

SHEM MI NATAKA FULL

THE CHIEFโ€™S DAUGHTER FULL

BIOLOGY TEACHER FULL