LOML | Love Of My Life (27)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:27
na kufoka nikisema β€œkumbe wewe mwanamke ni mpumbavu sana, ina maana hii ndiyo tabia yako G. Baada ya siku zote hii ndiyo tabia yako. Umenisikitisha sana, umekaa una nuna, umenibebesha mzigo na kuona nimekukosea, nimeumia na kulia nikijua nimemvaa na kumuingilia shetani kwenye kazi yake kumbe wewe mpumbavu unajua unachofanya.

Umenisikitisha sana Gabriella, kinyume, Mungu wangu, Mungu wangu. Nimeoa mwanamke wa namna gani mimi. Sasa siku zote hutosheki si ungeniambia kuwa mimi ni jini, mimi sio wa kawaida Ricky mimi mwenyewe ningeamua kama nakuoa au sikuoi.

Jitazame ulivyo, tazama ulivyo huendani na mambo ya ajabu unayonifanyia. G wewe sio mtu, sio mtu kabisa, na wewe sio aina ya mwanamke mimi nataka, ooh Mungu nisamehe mimi, nisamehe ni huyu mwanamke mshenzi dhambi zangu zote mpe yeye tafadhali. G!!, G!!, nimeumizwa na wewe, nimesikitika sana. Wewe ni shetani kabisa.”

Ungemuona Gabriella sasa anavyo lia machozi mengi usoni na ana tia huruma akisema β€œmume wangu tafadhali naomba tuzungumze, nakuomba sana.Nakuomba usiniambie maneno makali hivyo.”

Nilimtazama na kusonya halafu nikaendea kabati ili nivae vizuri niondoke zangu kwa maana nashindwa kabisa kukaa hapa. Kitu kingine kinacho nikera zaidi ni namna mara ya kwanza alivyo kuwa anaigiza kuwa mimi ndiyo mwenye kosa. Akanuna, nikawa nabeba na zawadi nambembeleza nanyimwa na unyumba mimi kumbe yeye anajua anachofanya. Ni mwanamke mpumbavu sana. Amenifanya mimi nifanye mambo ambayo sijawahi kuwaza hata mara moja kwenye akili yangu.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

LOML | Love Of My Life FULL

SHEMEJI UMECHOMEKA KWELI? FULL

TOBO LA PANYA FULL

KIBOKO YANGU FULL