LOML | Love Of My Life (31)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:31
Tuliingia ndani, mama yangu alinikaribisha kwa furaha sana. Akisema β€œkijana wangu huyo, karibu sana mwanangu. Nilikukumbuka sana kusema kweli.”

Baba akawa anacheka tu. Unajua vile kuigiza upo sawa na haupo sawa sio kawaida eenh. Ni kupambana sana basi nikawa naumia. Vile wazazi wangu wana furaha na mimi nipo tu hapo. Sina furaha yoyote ile.

Wakati mama na baba wana furahia kuniona wakizungumza hili na lie kuhusu mimi. Mimi nilikuwa natabasamu tu.

Na kisha nilimwambia mama yangu β€œnaweza kwenda chumbani kwangu mara moja?”

Mama alimtazama baba na kisha mimi akisema β€œhapa ni kwako mwanangu, chumba chako siku zote kipo kwaajili yako na hatujafanya chochote kwasababu kina vitu vyako utafanya mwenyewe unachotaka.”

Nilitabasamu na kusema β€œumefanya vizuri sana mama. Nitashughulikia mdogo mdogo lakini zaidi ninapenda kiendelee kuwa hivyo tu.”

Walitabasamu, niliinuka na kuingia chumbani. Nilipofika, nilisimama na kutazama chumba changu. Nilikumbuka nyakati zangu hapa. Palikuwa ni sehemu yangu nzuri ya kuwaza na kutafakari mambo.

Palikuwa ni pazuri sana. Na sasa naishi mbali na hapa, nyumba kubwa na nzuri, nyumba ndoto ya kila kijana lakini nyumba ile naishi na mwanamke ambaye naona kabisa ni mwiba mchungu kwenye maisha yangu.

Mwanamke mzuri lakini anayenitesa kihisia, mwanamke ambaye mpaka sasa bado sijajua nimuelezee vipi kwasababu ndiyo kwanza hili linanitetemesha. Inakuaje mke wangu anafurahia mapenzi ya namna ile na mimi sijawahi kufanya naye.

Hili liliniuma zaidi, mke wangu sijawahi mfurahisha mimi, kuna kitu ana furahia zaidi tena wakati ambao mimi ninapambana kumpenda, nina pambana kuhakikisha hii ndoa ina dumu. Kumbe najenga msingi kwenge ardhi ya maporomoko. Inaniuma.

Nilijikuta napiga magoti katikati ya chumba changu, nilishindwa kabisa kuzuia machozi yangu. Nililia kwa muda pale chini, kisha niliinuka na kufuta machozi huku tukio hili likijirudia sana kichwani kwangu.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

SIMULIZI YA INGIZA FULL

CHAGUO LA MOYO FULL

BINTI MDUNGUAJI FULL

JOGGING MASTER FULL