
LOML | Love Of My Life (33)

๐๐๐๐ (๐ณ๐๐๐ ๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐) โฃ๏ธ:33
Halafu alikaa pembeni yangu na alisema โninakufahamu mwanangu, nakuelewa sana mwanangu. Najua haupo sawa. Sijui nini kinaendelea kwako, lakini nataka nikuambie kuwa kila kitu kitakuwa sawa. Utakuwa na furaha tena.โ
Nilimtazama baba.Nilifuta machozi na kusema โnashukuru sana baba yangu, asante sana.โ
Baba alinitazama, halafu alisema โsisi ni wanaume mwanangu, niambie tafadhali. Ndoa yako ipo salama?โ
Nilijikuta natokwa na machozi na kusema nikijikaza โsijui baba, najitahidi nimpende mke wangu, najitahidi baba. Najikuta nashindwa kabisa sijui kama nitaweza baba, naona kuna mambo yananididimiza hata huu upendo ninaotaka kuuamsha.โ
Baba alinikumbatia na kusema โhapana kulia kijana wangu, hapana kulia. Nataka nikuambie kuwa ni sawa kabisa kujisikia hivyo. Tena sisi wanaume kuna muda mke wako unamuona tofauti kabisa.
Lakini kitu cha kufurahisha ni kuwa una pambana kumpenda. Ina maana mwanangu humpendi Gabriella?, mbona ulikuwa naye kwa mahusiano?.โ
Nilimtazama baba na kusema โni kweli baba, kama mpenzi, nilikuwa namfurahia kama mpenzi, sikuwa naishi naye baba.โ
Baba alinifuta machozi na kuniuliza โkuna tabia ambazo huzipendi mwanangu, au hufurahii tu au pengine kuna mwanamke una mpenda?โ
Nilimtazama baba yangu, nilimtazama nakosa jibu. Kuhusu kuto mfurahia, kusema kweli kuna vitabia vyake tu vinanikera lakini kubwa zaidi simfurahii kama mke wangu na mbaya ni huu wakati napambana niweze kumpenda nagundua mambo mengine mabaya. Kuhusu mwanamke mwingine mimi sina, ingawa nilimuona na kumfurahia ila sio wangu na wala sipo naye.
Baba alinishika mkono na kusema โmwanangu, kijana wangu. Nimekulea kwa upendo sana. Nimeshuhudia hatua kwa hatua unakua kijana mzuri na mimi nikiwepo. Wewe ni kijana mzuri na mwenye hofu ya Mungu ndani yako. Hii ni ndoa yako mwanangu, ndiyo ya ujana wako. Umepata mke mzuri wa ujana wako.

