
LOML | Love Of My Life (34)

๐๐๐๐ (๐ณ๐๐๐ ๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐) โฃ๏ธ:34
Kitu pekee unatakiwa kufanya kijana wangu ni kuipambania ndoa yako, kuhakikisha kฤฑla kiti kinakuwa. Sio rahisi mwanangu tena wakati mwingine ni ngumu haswa. Lakini usikubali kushindwa wewe ni mwanaume na ndoa yako hata mwezi bado tafadhali. Simama imara.โ
Nilimtazama baba na kujikuta namuuliza โumewahi kukaa siku ukajutia kumuoa mama yangu, au kuhisi humpendi kabisa?โ
Baba alinitazama kwa muda, nikaona macho yake yakibadilika. Halafu baba yangu alitazama chini. Nikaona anainua mikono yake na kujifuta machozi. Halafu nikaita โbaba!!โ
Baba aliinua uso wake akitabasamu japo naona hayupo na tabasamu La awali na kusema โkuna mtu kijana wangu huna La kufanya kabisa una acha tu maisha yafanye vile yanataka. Ndiyo maisha. Inatokea Mara nyingi lakini sio sababu ya kuacha ndoa yako. Wakati mwingine suluhu ni kutulia tu.โ
Nilimshangaa baba yangu, wakati huo mlango ulikuwa unafunguliwa, alikuwa mama akitabasamu na kusema โbaba na mwana, mna kikao gani cha Siri namna hiyo?โ
Tulijifanya kucheka tu, halafu mama aliniuliza โUpo sawa lakini?โ
Nilitabasamu na kusema โkabisa mama, hata hivyo nataka niwahi nyumbani.โ
Mama alitabasamu na kusema โkabisa maana binti yangu alipiga anaonekana na wasiwasi sana. Kฤฑla kitu kipo sawa lakini.โ
Nilimtazama mama na Kisha baba nikainuka pale nikisema โkila kitu ni sawa kabisa. Baba uwe na usiku mwema, mama yangu Nakupenda sana. Mimi niwaache sasa.โ
Sikusubiri hata jibu, nikawa natoka huku nasikia mama anaita โRodricky, wewe Rodricky, Ricky mwanangu.โ
Baba ana mwambia โmke wangu, Muache mtoto. Muache aende.โ
Sijui waliendelea kuzungumza nini, mimi niliingia kwa garฤฑ yangu, niliwasha garฤฑ na kuanza safari ya kutoka pale nyumbani.

