LOML | Love Of My Life (35)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:35
Nikiwa nishatoa gari nilichukua simu yangu, lengo lilikuwa nimtafute Willy, pengine Labda nitaweza kuongea naye. Nilichukua simu. Nilikuta mke wangu amenipigia sana. Missed call nyingi sana. Nilitazama na kushika simu yangu kwa nguvu zote. Nilikuwa natamani kama yeye ndiyo awe ile simu lakini inawezekana vipi.

Nilitazama machozi yanatoka. KΔ±la nikikumbuka vituko vya nje wangu ndiyo nazidi kuumia. Aliniandikia ujumbe akisema β€œDadie tafadhali, nakuomba sana, usinifanyie hivyo. Wewe ndiyo kila kitu nahitaji, wewe ndiyo sababu nipo hapa leo.

Hujui tu ni namna gani umenisaidia, uwepo wako umeongeza mengi sana kwenye maisha yangu. Wewe ni nuru yangu, mwanga wangu Ricky. Nakuomba tuzungumze, nakuomba mpenzi, mume wangu nisikilize nakuomba sana. Haki ya Mungu Nakupenda sana.”

Sikutaka hata kuhangaika naye, nilimpigia simu Willy. Alipokea na aliniita β€œkaka niambie.”
Nilikosa cha kusema hata akasema β€œhello, kaka unanisikia?”
Nilijikaza na kumuuliza β€œupo wapi bro!!”
Willy aliniambia alipo akisema β€œsina muda mrefu hapa, kuna vitu wife aliniagiza namchukulia Kisha narudi nyumbani.”
Nilivuta pumzi na kusema β€œnisubiri.”
Willy aliniuliza β€œKwema kaka?”
Mimi nilikata simu yangu, nilipokata tu simu ya mama yangu iliingia. Nilipokea, mama yangu aliniambia β€œmwanangu mwenzio yupo hapa wewe upo wapi tena?”
Nilishangaa, Ina maana mke wangu amenifuata mpaka nyumbani. Nilimwambia mama β€œmwambie arudi nyumbani mimi narudi sio muda.”
Mama aliniuliza β€œkuna usalama lakini?”
Nilimwambia mama yangu β€œkila kitu kipo sawa mama.”
Mama alisema kwa upole β€œsawa mwanangu, ninawaombea sana, mpendane na kusikilizana. Ndoa yenu idumu milele.”
Nilivuta pumzi ile kujibu amina mpaka machozi yaani β€œamina mama.” Na machozi juu.

Nilikuwa nashindwa kuelewa ni mwanamke wa aina Gani nimeoa. Mwingine kwake ni kawaida Labda pengine kwasababu siku hizi mambo haramu yana kuwa mazuri na kupigiwa kampeni.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata