
LOML | Love Of My Life (37)


𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:37
Nilisema kWa upole “hata sijui kaka sielewi mimi.”
Willy aliniambia “unaweza kuniambia chochote tafadhali.”
Nilimtazama na kusema “kaka nisamehe sana nimekusumbua. Nisamehe sana. Naomba niende wahi nyumbani.”
Willy alitikisa kichwa na kusema “sijui tatizo lako Ricky, nashindwa namna ya kukusaidia. Unajua hili ndiyo tatizo letu wanaume wengi sana. Kufunguka, kuwa wakweli, kuzungumza mambo yanayo tusumbua.
Sijui ni gümü namna gani lakini kitu naweza kusema rafiki yangu ni muulize Mungu ufanye nini?, Mungu atakupa majibu, siku zote Mungu ana majibu ya maswali yetu magumu. Njia nyingine ya kutatua matatizo ni kuzungumza rafiki yangu.
Kama ni mke kaeni chini mzungumze msikilize na umuelewe. Tatueni matatizo yenu pamoja, amueni pamoja na Mvuke pamoja. Sisi bado Vijana ninayo imani unanielewa tena bahati nzuri tunajitambua na kuelewa maisha.
Usitumie hasira, kuwa mpole, fuatilia jambo na ulielewe. Nina hakika Mungu hataki ndoa zivunjike lazıma utapata suluhu.Tafadhali sana ndugu yangu jitahidi kwenye hili na Kama bado huelewi mimi ndugu yako nipo. Nitakusikiliza na nitakuwa na wewe kuzungumza kuhusu lolote lile tena kwa kına kabisa. Nakuomba sana usijiumize kihisia bado tunakuhitaji.”
Nilimtazama na kusema “nashukuru sana kaka, sijasema nini kinanisumbua lakini umezungumza na mimi vizuri sana. Nimejisikia vizuri sana. Nashukuru sana kaka. Nimependa vitu umeniambia nakuahidi nitashughulikia hili na nitarudi kwako. Nashukuru sana kaka. Naomba nirudi nyumbani sasa.”
Willy aliniuliza “una Hakika upo vizuri au nikusindikize?”
Nilimtazama na kucheka kidogo nikisema “muwahi shemeji kaka, na Mimi nimuwahi nyumbani.”
Wakati huo simu yangu iliita, wote tulitazamana na Willy akasema “Shemeji yangu huyo anapiga haya ongea naye sasa.”
Nilimtazama tu huku moyoni nikisema “ungejua kinachofanya anapiga simu wala hata usinge niambia haya.
Sikupokea ile simu kabisa, wakati ndiyo Nawashukuru garı rafiki yake alinipigia simu. Niliitazama na Kisha nilipokea, alipokea na kusema “Shem lake upo sawa?”
Nilimwambia kWa upole “nipo salama kabisa Shem.”