
LOML | Love Of My Life (39)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:40
Mke wangu alikuwa anapiga sana simu, simu ilikuwa inaita sana lakini sikuwa najali. Sikuwa napokea. Meseji ndiyo usiseme. Mke wangu analalamika βbaby please, nakuomba mume wangu nimeenda mpaka nyumbani sijakukuta. Upo wapi mume wangu. Tafadhali nakuomba.β
Text na emoji za kulia Kama zote. Mimi ninatazama tu simu na Nakumbuka mida ya saa tano hivi ndiyo nilianza safari ya kurudi nyumbani.
Nilifika nyumbani, nilichelewa kusema kweli na kuchelewa nyumbani sio kitu mimi Napenda Ila imekua na sina namna. Nilipofika nikaingia ndani. Nilipoingia tu nilimkuta Giana na rafiki yake akiwa Analia. Giana aliponiona alinitazama kwa upole na kusema βShem Karibu.β
Niliitikia kwa ustaarabu kabisa βAsante shem, upo hapa.β
Giana aliniambia βsikuwa na namna niliona nije tu Ila kwakuwa umefika Naomba niwaache please shem zungumzeni.β
Mke wangu alisimama na kusema kwa upole βkaribu mume wangu.β
Nilimtazama tu, Kisha nilimwambia Giana βnikupeleke ni usiku sana.β
Giana alinitazama na kusema βUsijali Shem, mume wangu atanifuata tu hakuna shida. Hayupo mbali na hapa ndiye alinileta.β
Nilimtazama na kusema βpole kWa usumbufu, karibu sana utamsalimia sana bro.β
Giana alisema kwa upole akitoka βAsante sana shem, Rafiki yangu uwe na usiku mwema. Tafadhali zungumza vizuri na mumeo.β
Sikujibu kitu badala yake mimi nilianza safari ya kuelekea chumbani. Haraka mke wangu alipiga magoti na kushika miguu yangu akilia kwa maumivu akisema βmume wangu tafadhali nisamehe, nakuomba mume wangu.β