LOML | Love Of My Life (42)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:42
Mbaya zaidi na mimi nilikuwa naona ule ndiyo upendo, nilikuwa naona yale ndiyo maisha yangu. Nilikuwa nampenda sana, nilikuwa nampenda siwezi kumuacha kabisa.

Sikuwa naweza hata kuwa na mwanaume mwingine kabisa alikuwa ni yeye tu. Familia yangu ilihangaika sana kunitoa kwake, hata nilihamishwa nchini na kwenda kusoma mbali.

Niliteseka, nilikuwa sioni baya kwenye kΔ±la kiti sisi tuliona ni mapenzi hata hivyo tulikuwa tunapendana sana mbali na changamoto zote. Mwaka mmoja baadaye niliona kwenye matangazo ya vyombo vya habari kuwa amehukumiwa maisha.

Habari ile ilinila sana. Nililia sana, nilihangaika sana hata nikarudi tena nchini. Nilianza kugundua kuwa nilikuwa nakosea. Taratibu nilianza kukubali ile hali, nilianza kujipenda na kujifurahia. Miaka miwili mbele aliugua na kupoteza maisha kwani alikuwa ameathirika sana na madawa.

Ricky ni hadithi ndefu lakini niliamua kujipenda na kuacha kila kitu mpaka nilipokuwa na wewe hapo. Ukafanya safari yangu ya uponyaji kuwa rahisi.Nilianza kupona, nilianza kukupenda na nakupenda sana. Unanitosha, unatosha sana Ricky mpenzi, bado nakuhitaji sana, usiniache tafadhali.

Najua nimekukosea, sitaki hata kujielezea sana. Ni kitu kibaya sana nimekosa mpenzi. Lakini unajua kuwa nakupenda, unajua kuwa siwezi kuishi bila wewe Ricky, mimi ni kichaa, kichaa wa penzi lako.

Nakuahidi sitakuwa hivi tena, ninabadilika sana na nimeweza na wewe najua utakuwa kiongozi wangu mzuri sana. Am sorry Baby, Dadie nakuomba tafadhali nisikilize mimi, nisikilize usiniache nakuomba sana, nakuomba.”

Alikuwa analia sana, ukimuona ni kama sio Yule mdada mrembo, mdada wa kΔ±sasa. Alilia kWa uchungu sana nilikuwa namuhurumia lakini sikutaka aone huruma yangu.

Nilimwambia nikisema β€œGabriella hata ulie namna gani, kitu umenifanyia ni kibaya sana. Tena umenichefua akili yangu, umefanya nikuone wa ajabu sana. Na mbaya zaidi ukajifanya kuonewa. Wewe ni mwanamke wa aina gani lakini?, Ina maana mpaka leo hujui hiyo ni mbaya sana mbele ya Mungu, wewe mwenyewe unaona ni ujanja huwazi hata madhara yake kiafya.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

UTAMU WA JAMILA FULL

SHEM MI NATAKA FULL

BINTI MDUNGUAJI FULL