LOML | Love Of My Life (43)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:43
Kuna mambo unaona ni hayaendi au ni maisha yangu yanarudia kitu kilekile kwasababu ya huo upumbavu, msomi kabisa unaye elewa mengi kuhusu kujitambua bado unafanya huu upumbavu umenisikitisha sana na unataka unifundishe na mimi sasa ili na kizazi chetu kiwe cha shetani.”

Mke wangu alilia kwa uchungu akisema β€œNimekosa mume wangu, Nimekosa nakuomba sana. Na apa kwa Mungu, kwaajili ya huyu mtoto tumboni, kwaajili ya kΔ±la kitu, na hata kama nikiendelea hivi mimi mama yangu afe, niamini mume wangu naacha kabisa hata hivyo sifanyi hivi tangu nimekutana na wewe.

Sijui hata imekuaje najisikia aibu, najisikia vibaya, nateseka sana, naona nimefanya koşa kubwa maishani haswa kwako mpenzi wangu wa maisha. Nakuomba nitazame, nionee huruma mimi, siwezi kuishi bila wewe, siwezi kuishi ni Bora kufa kuliko kukukosa maishani.”

Kusema ukweli alitia huruma sana, alikuwa analia mpaka kamasi. Nilijikuta namuinua nikisema β€œGabriella wewe ni binti wa kikristo. Mzuri kabisa umefundishwa upendo na maana halisi ya maisha ya duniani. Ulibatizwa ili umfuate Kristo na mambo yake.

Ninazo dhambi ndiyo, ninatubu sawa. Lakini hii dhambi ambayo Mungu aliharibu kabisa ulimwengu wake, kizazi chake inatafuta nini kwenye maisha yako. Ina maana hujui hadithi hizi?, hujawahi kusikia ilikuwa vipi?.

Au unafikiri Mungu haoni na hawezi kuangamiza ulimwengu kwasababu ya mambo haya. Mungu ataangamiza ulimwengu wako, kila kilicho chako, kitaenda kizazi na kizazi hata ambao hawapo sasa watalipia makosa yako, hivi ndiyo unataka?, watoto wetu wateseke kwasababu yako.

Mimi sijui utafanya nini, ila una hitaji muda na Mungu, sijui kabisa, umenisikitikisha sana, sijategemea kama unaweza kufanya huu uchafu. Nisikilize sitaki unisumbue, Niache kama nilivyo tafadhali, usiniulize kitu chochote sijui hata kama unanielewa?”

Akiwa ameinamisha kichwa chake alisema akiwa analia β€œnajua nimekutia kinyaa, najisikia maumivu, nateseka sana mume wangu. Nisamehe Mimi, nakuomba mume wangu. Sina hata neno zuri La kusema.

Nisamehe usinipe adhabu kubwa namna hiyo ya kutokuwa karibu na wewe na wewe ndiyo kila kitu kwangu. Nakuomba sana, nakuomba tafadhali.”

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

SHEMEJI UMECHOMEKA KWELI? FULL

UTAMU WA JAMILA FULL

BIOLOGY TEACHER FULL

UKO HOME NIJE FULL