
LOML | Love Of My Life (46)

ย
๐๐๐๐ (๐ณ๐๐๐ ๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐) โฃ๏ธ:46
Nilipokuwa nawaza hayo usingizi ulinichukua tena. Safari hii niliamshwa kwa upole na sauti ya Gabriella mke wangu. Aliniita kWa upole โMume wangu!!, Mume wangu!!, amka kipenzi chai ipo tayari.โ
Nilipo fungua macho yangu nilimuona akiwa amependeza mwenyewe unajua ni mrembo sana. Nilimsalimia kwa upole โGoodmorning!!โ
Alitabasamu na kusema kwa upole โMorning hubby, umeamkaje Dadie?โ
Nilimtazama na kushusha pumzi nikisema โnipo salama kabisa.โ
Baลฤฑ niliinuka na Kisha kutazama muda, ilikuwa ni saa nne asubuhi. Nilisema kWa sauti ndogo โnimechelewa, tangulia nakuja.โ
Alinitazama na Kisha aliniambia tena โMume wangu kipenzi, tafadhali nisamehe sana. Ninajitahidi kuwa mke mzuri kwako. Nakuomba nisamehe Nipe nafasi nyingine.โ
Nilimtazama pasฤฑ kusema kitu na yeye akawa anatoka na mimi nilishusha pumzi na kuingia bafuni. Nilijiweka safi haraka haraka na nilitoka kwaajili ya kupata chai. Na wakati nimefika mezani Yule alikuwa anamalizia kuweka meza sawa na kuondoka zake. Niliita โmama Babuu!!โ
Alinitazama na kusema โNaam boss!!โ
Nilitabasamu na kusema โkwanini usikae hapa tule pamoja na badala ya kila siku kula ukiwa jikoni.โ
Mke wangu alinitazama na kusema akitabasamu โmume wangu Muache tafadhali, alishakunywa chai hata hivyo ana kazi za kufanya. Nataka kuzungumza na wewe hapa mpenzi.โ
Nilimtazama tu mke wangu, nina mjua ni mtu wa nyodo. Kukaa hapa na mama Babuu hata asingesema kitu asingependa tu kwasababu haijawahi kuwa. Kitu ambacho naona familia nyingi hata kwetu pia yaani sijui inakuaje.
ย

