
LOML | Love Of My Life (47)

๐๐๐๐ (๐ณ๐๐๐ ๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐) โฃ๏ธ:47
Nilijifunza upendo kwa familia ya Willy. Wanaishi vizuri sana. Nilitamani na mimi nianzishe utaratibu huu kwangu. Lakini hata mama Babuu mwenyewe ni wazi hawezi isitoshe wanajuana wao.
Lakini Labda mimi sasa ndiyo sielewi, mkiishi kama familia na kula mezani pamoja kuna shida gani?, haibadilishi wala haiharibu kitu zaidi ina dumisha upendo ndani ya familia na mnaishi na furaha pamoja.Sio mke wangu, kazฤฑ za nyumbani hizi sio mambo yake kabisa.
Nilianza kula, vile naanza tu simu yangu iliita. Alikuwa ni Willy, nilipokea simu nikitabasamu na kusema โkaka!!, kaka!!, niambie ndugu yangu.โ
Willy alisema โLeo umefurahi sana, unaendeleaje?โ
Nilitabasamu na kusema โsalama kabisa kaka, tutaongea usijali.โ
Akaniambia kWa ucheshi โHakuna shida msalimie shemeji yangu.โ
Nilimtazama mke wangu na kusema โHakuna tatizo nitamsalimia na ipo siku nitamleta.โ
Willy alisema โnitafurahi sana kusema kweli karibuni sana.โ
Nilimjibu kWa uchangamfu โnashukuru sana. Karibu.โ
Nilikata simu, mke wangu alinitazama na kuniuliza โni nani mume wangu?โ
Kwa kifupi tu nilimjibu โrafiki yangu.โ
Halafu niliendelea kula, nilikula na alinitazama na kusema โMume wangu tafadhali usiwe hivi.โ
Nilimtazama na kusema โGabriella tafadhali unaweza kuacha kusisitiza. Nitakuwa sawa, nitakuwa sawa unatakiwa kujua sijisikii vizuri unanielewa.โ
Mke wangu alinitazama tu na Kisha kwa upole aliinuka. Nilijua tu amenuna na anavyo penda kudeka lakini kiukweli siwezi kujilazimisha kuwa nina furaha wakati ninaugua ndani kwa ndani. Hivyo nilimuacha aende

