
LOML | Love Of My Life (48)

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:48
Maisha yangu yalianza hapa na mke wangu. Mke wangu alitoka kwenda kazini na mimi nilitoka kwenda kazini kwangu. Alikuwa ananipitia kazini, ananiletea na zawadi basi vile akiingia ofisini amependeza watu wanaona boss kapata kumbe wala hata simgusi mke wangu kabisa yaani.
Akifika anasema “baby nimekuletea zawadi nzuri sana, tafadhali pokea.”
Natabasamu napokea, ananiuliza “mume wangu umeipenda?”
Namwambia kWa tabasamu “Asante mke wangu ni nzuri sana, nimeipenda.”
Başı ananiambia “tukale tafadhali dinner mpenzi.”
Namtazama tu nasema “ni sawa mke wangu.”
Başı tunarudi nyumbani tunapendeza tunakula lakini ndani simgusi kabisa. Siku zilienda huko chumbani mke wangu anajitahidi kunivalia vitu vizuri lakini mimi nafsi yangu imeingia nyongo kabisa mpaka siku hii.
Ilikuwa tumetoka Dinner tumependeza. Tulipofika nilivua nguo nikaingia kuoga na mke wangu alifuata Baada yangu. Alitoka akiwa amevalia nguo nzuri ya kulalia. Nilimtazama na kusema “umependeza sana Gabriella.”
Alitabasamu na kusema “kila kitu nafanya kwaajili yako mpenzi.”
Nilitabasamu, na Kisha alianza kunifuata na Kisha alinipa mdomo wake. Siku hii nakiri ni wazi alipania sana. Alianza kunipapasa sehemu anajua mimi ni dhaifu, alinifunua ile gauni yake na kukaa mapajani mwangu akinibusu.
Ghafla nilijikuta nakwepa nikisema “nimechoka sana Gabriella nataka kupumzika.”
Gabriella alinitazama na kusema “this is not fair. Sio haki kabisa Ricky. Ni nini unafanya. Una maana ninavyo kuomba msamaha hunielewi, ni nini sasa kujifanya umenisamehe. Najaribu kila kitu kuhakikisha nakuwa bora, nakupa furaha, najenga Tena nyumba yetu.

