
LOML | Love Of My Life (54)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:54
Alitabasamu na kusema βnashukuru sana mume wangu, nashukuru sana. Nakupenda Ricky wangu.β
Nikatabasamu na kumuinua pale na tulianza kuelekea chumbani kwetu.Baada ya kufika chumbani hasira zote nilitupilia mbali, nilitaka kuhakikisha mwanamke huyu anakuwa salama, nampenda na tunaanza upya. BaΕΔ± siku hii hata tulioga pamoja kwa furaha kabisa.
Na mke wangu akiwa mwilini mwangu aliniambia βmimi ni mwanamke mwenye bahati sana kupata mwanaume kama wewe. Nashukuru sana kwa kunipenda, Asante kwa kunichagua na kunifanya wako.
Sio mkamilifu sana ila kwaajili yako nitapambana kuwa mke sahihi, mke ambaye ulikuwa una muota. Mimi nakupenda sana mume wangu, nakupenda maisha bila wewe hakuna kitu. Nakupenda kiasi kwamba natamani dunia yote ijue wewe ni wa namna gani. Nakupenda sana mume wangu.β
Nilitabasamu na kusema βhata mimi Nakupenda sana mke wangu. Nitafurahi kama utakuwa mke mzuri sana kwangu na mtoto wetu. Δ°mani yangu ni kuwa tutakuwa na familia nzuri yenye kupendeza.β
Mke wangu alitabasamu tu, Kisha yeye alitoka na mimi nilibaki bafuni namalizia kuoga.
Nikiwa bafuni namsikia tu huko akiwa na furaha sana anazungumza na simu akisema βmimi mume wangu ananipenda sana, unajua mume wangu anaweza kufanya lolote kwaajili yangu. Mume wangu ananidekeza sana.β
Halafu anacheka, Nilitikisa tu kichwa nikisema βwanawake bhana.β
Mke wangu ni mtu wa mume wangu, mume wangu hivi, mume wangu vile, mume wangu kafanya hiki, mume wangu kaniletea hiki na kile hii ni tangu mahusiano.