LOML | Love Of My Life (55)

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:55
Sio kitu kibaya lakini nafikiri mtu ukipendwa vizuri hata usiposema watu wao wenyewe watajua tu kuwa una amani na furaha kwa maisha yako.

Hii mume wangu amefanya hivi, mume wangu hawezi nisaliti, mume wangu ameleta hiki, kikapanda kikashuka ni kama kutangaza vita na shetani.

Kwasababu hujui mtu unamwambia, una muelezea ni nani, anawaza nini kwaajili yako. Watu wengine maneno yao tu ndani ya moyo ni mabaya juu yako.

Kama ilivyo pesa inakaa kwenye heshima na ndoa hivyohivyo inalindwa kwa heshima. Ni vizuri sana kuheshimu kila kitu na sio kumkaribisha shetani.

Nilitoka zangu bafuni, mke wangu alikuwa na furaha na kusema vile anaongea na rafiki yake akimtaja jina lake “Giana huyo!!”
Nilitabasamu na kusema “anasemaje shemeji yangu.”

Alinitazama na kusema “atasema nini tena, leo anatoka na mume wake basi ananitambia.”
Nilitabasamu nikisema “wewe sasa unatakiwa kutulia mpaka ujifungue nitakupeleka Paris.”

Mke wangu alinitazama na kusema “mmh unanitania si ndiyo?”
Nilicheka na kusema “kwanini nikutanie, nataka kukufanya mwanamke mwenye furaha hapa duniani. Nataka nikupende sana Gabriella. Wewe ni mke wangu.”

Mke wangu kwa madeko alisema “wako, peke yako, waoooo nasubiri kwa hamu. Nijifungue tu jamani.”
Nilicheka nikisema “mpaka mwisho wa mwaka huko, tulia tu.”
Alisikitika kidogo na kudeka akisema “hata hivyo sio mbali, nitafika lazima. I love you Dadie.”

Nilitabasamu na kusema “I love you mamie.”
Alinikumbatia na kunibusu. Unajua tena watoto wa wenye pesa madeko madeko tena hapa ndiyo kwake. Gabriella wangu anadeka sana.

Başı siku hii ilikuwa siku nzuri sana, siku yenge furaha, maana tulifanya kila kitu ambacho ndoa yenye furaha inatakiwa kuwa nacho. Nyumba ilitabasamu, ilishangilia nyumba ilikuwa nzuri sana nakumbuka.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata