
LOML | Love Of My Life (58)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:58
Mke wangu aliinamisha tu kichwa chake, nami nilifanya kwa mapenzi nataka mtoto wangu awe salama sitaki madhara. Nilibeba furushi hili La misumari ningefanya nini sasa. Niliumia ila kusema ukweli nataka mtoto wangu azaliwe na afya njema kabisa.
BaΕΔ± nilisema βni ujinga tu na sasa natambua sikuwa sahihi, tafadhali kaka unaweza msaidia mke wangu.β
Dokta alitabasamu na kusema βusijali maadamu umekuwa muwazi utaniruhusu nimkague mgonjwa wangu na nijue naanza kumsaidia vipi akae sawa.β
Nilimtazama mke wangu na yeye hakuwa ana amini hili. Kweli sikuwa na La zaidi niliacha dokta afanye anachofanya. Baada ya muda walimaliza tulipewa dawa na alisema mke wangu Baada ya matibabu ambayo ameanza kumfanyia basi kila kitu kitakuwa sawa kabisa.
Nilifurahi na kumshukuru sana daktari na Baada ya hapo sasa nilimshika mkono mke wangu. Tulitoka na hatukufika hata mbali mke wangu alisimama na kusema βmume wangu, kwanini umeamua kunifanyia hivi, sio wewe, sio koΕa lako kwanini?β
Nilimtazama na kusema βmke wangu, nawezaje kumwambia dokta mwanaume mwingine ndiye amefanya hivyo?, eenh nawezaje mke wangu. Ninakupenda, nakujali wewe na mtoto. Nataka mtoto wangu azaliwe salama, nataka awe salama kabisa.β
Mke wangu alinikumbatia, na Mimi nilisema βtulia mke wangu, una stahili hili. Siwezi kukusababishia aibu kama aibu na itupate wote ili tuwe salama na mtoto wetu si unaona mmetibiwa.β
Mke wangu alisema βhata sikuwa najua kuna matibabu sema umenishangaza mume wangu naona aibu kabisa.β
Nilimwambia mke wangu βnataka uwe salama wewe na mtoto kwaajili yangu.β