LOML | Love Of My Life (59)

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:59
Alinibusu na kwa kushikana mikono tulielekea gari na safari ilianza. Tulipita madukani kidogo kısha alinunua alichotaka nami nikamwambia nampeleka kwa rafiki yangu.

Alifurahia na vile anapenda kujulikana ni Mrs Rodricky ndiyo basi tena. Na safari ilikuwa ni nyumbani kwa Willy.Tulifika tulikuta Willy na mke wake wanafua.
Nilitabasamu, nilifurahi kuwaona namna ile.

Nilisimamisha gari na kumfungulia mke wangu mlango. Akashuka. Walifurahi sana kutuona na Willy alisema “aanh kaka suprise gani tena hizi si ungesema tu.”

Mimi Nilicheka, mke wake na yeye alimkaribisha mke wangu ile furaha unaona wazi. Lakini Baada ya muda niliona mke wangu na mke wa Willy wanaingia ndani. Willy alinitazama na kusema “wewe mjinga una bonge La mke cheki Toto.”

Nilicheka na kusema “wako umemuona bro, bonge La kitu.”
Hadithi za wanaume tena unajua, Willy tunaenda kukaa huku ananiuliza “mnaendeleaje naona mna furaha.”

Nilitabasamu na kusema “Asante kWa ushauri wako kaka. Naona ninaweza. Nimekubali ni mke wangu ni mzuri hivyo ingawa nasukumwa sana moyoni kumfuatilia naona kuna vitu sielewi lakini huu sio muda wa kuzungumza si unajua tena mazingira.”

Na kweli wakawa wanatoka sisi tunacheka tu. Başı mke wangu aliketi mke wa Willy yeye akasema anaingia ndani. Tuliongea hili na lile pale muda wote mke wangu na simu. Sikutaka Mzuia nikawa tu nacheka. Ulipita muda Willy na yeye akaingia ndani.

Nilimtazama mke wangu alitabasamu na kusema “ni pazuri, rafiki yako ni mcheshi na anampenda san amke wake.”
Nilitabasamu na kusema “sana si unaona walikuwa wanafua wenyewe.”

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata