LOML | Love Of My Life (61)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:61
Baada ya muda mke wangu alirudi akisema β€œmume wangu ukimuona mama babuu, amefurahi kama nini!”
Nilicheka tu. Kusema kweli nyumba mkiwa na furaha inakuwa nzuri sana. Siku hii iliisha vizuri hata kesho yake mke wangu alisaidiana na mama Babuu wakaandaa chakula, mke wangu alinifulia nguo zangu za ndani hata mama babuu bila Shaka alishangaa na pamoja tulikaa mezani. Niliwasifia sana kwa chakula kizuri mke wangu alifurahi sana. Alifurahi mno.

Maisha yaliendelea, mke wangu aliwahi kuamka kwenda kazini hata siku hii nilimwambia β€œmke wangu kwanini usipumzike mpaka ukijifungua.”

Alinitazama na kusema β€œhapana baby wangu, mimi kukaa nyumbani sitaweza kabisa, Acha tu nikichoka nitapumzika uzuri ni kuwa hatujaajiriwa na si unajua tulipata hasara hivyo kurudi pale ni lazima nipambane.”

Nilivuta tu pumzi na kusema β€œni sawa mke wangu, ni sawa.”
Başı kazini tunapelekana na kupitiana kurudi. Tunanunuliana zawadi na mambo Kama haya. Hata kuhusu Yule msichana sasa Hapana Tena nimejikita na mke wangu na nahakikisha dawa anatumia vizuri kila kitu kilikuwa kizuri.

Lakini ule uvivu wa mke wangu wa ibada ukafanya hata kanisani tunaitumia kama mapumziko. Ndani ya nyumba mke akiwa mvivu kuomba au kwenda kanisani hiyo nyumba ni sawa na kuzimu au uwanja wa fujo zote za duniani.

Ni lazima mke awe amejitoa sana kwaajili ya familia ili nyumba iwe salama sio kwamba wanaume hawatakiwi kusali. Lakini wanaume wachache sana wana moyo wa kuomba, wengi wanategemea mwanamke na Mimi nilikuwa mtu wa kanisani vizuri lakini mke wangu hapendi kwenda kanisani ile uvivu ukaja na kwangu na sina tena matumaini ya kumuona mrembo Yule wa kanisani nishaamua ninampenda mke wangu.

Maisha yalikuwa safi kabisa, sasa ni miezi mitatu tangu tufunge ndoa, mimba inazidi kukua ingawa sio sana ila ukimuona tu unajua huyu ana mimba. Hatukugombana tena, kila kitu kilienda vizuri sana. Ukawa mwezi wa nne hospitali namsindikiza vizuri kabisa na dokta yuleyule.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata