
LOML | Love Of My Life (65)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:65
Nilitoka sikusubiri maelekezo. Nilipokuwa njiani nililia kama mtoto, nikikumbuka zile meseji nachukua simu yangu nasoma nacheka huku nalia naonekana kama mpumbavu vile.
Mtu nimeamua kujikana nimpende Kumbe hastahili. Kuna watu ni wazuri kwa nje ndani wameoza ndiyo mke wangu na upole wake ule ucheshi hafananii.
Ameoza ananuka, simu ya mke wangu ni chafu sana. Ni chafu mno. Roho inaniuma kusema ukweli, zile picha na Mc wa ndoa yetu jamani Mpaka ofisini. Mimi siku ya ndoa nipo pale Kumbe Kama kituko. Sasa hii ni ndoa ya aina gani, ndoa takatifu au ndoa takafujo.
Nilikuwa nalia kama mtoto. Nilijikaza na kumpigia simu huyo Max. Aliniambia kWa upole βnina kazΔ± kanisani kaka ndiyo namalizia hapa tutaonana baadaye Labda.β
Nikamuuliza kWa upole βkanisa gani kaka ni muhimu.β
Alikuwa kule tumefungia ndoa.
Nilimwambia kWa upole huku mimi nalia βnakuja kaka, tafadhali nisubiri.β
Niliendesha garΔ± kWa kaΕΔ± sana, tena huku nalia kwa hasira nikikumbuka namna nimejitahidi kuokoa ndoa yangu. Nilifika kanisani, nilimwambia Max anifuate nilipo. Alipofika niliingia kwa gari, alipoingia mimi nilikuwa nimeinamia usukani. Aliniita βkaka, upo sawa?β
Niliinua uso wangu taratibu, uso umejaa machozi, uso umechoka, uso una maumivu, na si kupoteza muda nilimuuliza βkwanini unatembea na mke wangu Max, kwanini unalala na mke wangu?β
Niliona Max akitetemeka, sijui hata nilifanyaje, nilishindw kujizuia nikajikuta namkaba kwa nguvu, Max alianza kutetemeka akilia huku anasema βtuzungumze kaka, nisamehe ni mkeo ndiyo ananitaka mimi, nielewe kama nisamehe.β