
LOML | Love Of My Life (66)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:66
Nilizidi kulia kwa hasΔ±ra nikisema βnakulisha wewe na familia yako, nakuona kama kaka, msimamizi wa ndoa yangu. Kumbe hufai, leo nitakuua wewe halafu nife mimi, unalala na mke wangu, tena unalala naye namna mimi silali naye, unamuingilia mke wangu kinyume na maumbile vyovyote unachotaka unapata, unajiona kidume sio. β
Max alikuwa anahangaika mpaka mkojo unamtoka, kosa langu na bahati yake sikulock milango, alifanikiwa kufungua tukaangukia nje watu wanatushangaa wale wachache waliopo nje.
Max palepale alifanikiwa kunikimbia, nilibaki nalia kwa maumivu makali sana ndani ya moyo wangu nikisema βnooooo!!, hapana, inauma sana, naumia.β
Wanaume wawili walinichukua kwa upendo tukaingia kanisani. Baada ya kuingia kanisani walinituliza lakini sikuwa naweza kutulia, nilizidi kulia kwa uchungu nikiwa nimepiga magoti.
Nililia nikisema βMungu wangu kwanini Mimi, kwanini Mungu, ni ndoa gani ya mateso hii umenipa kwanini, usaliti wote huu kwanini Mungu wangu?β
Nilikuwa nalia kwa uchungu sana. Wakati nalia nilisikia sauti nyuma ya mwanamke akisali kwa utulivu alisema maneno haya Nakumbuka sana, alisema βMungu baba yangu wa Mbinguni, umenibariki kwa namna nyingi sana na nakushukuru sana.Ninatambua mipango yako juu ya maisha yangu ni mikubwa na inapita uelewa wangu.
Naomba uniongoze na uzidishe imani yangu kwako baba yangu.Ninaweka maisha yangu, Δ°mani yangu, kazi yangu, mtoto wangu, na kesho yangu nisiyo ijua mikononi mwako.
Ulinivusha na Yale, ninakuamini sana kwenye haya, nina imani na wewe bila wasiwasi wala kusita.Ongoza maisha yangu na wote walio nizunguka.
Adui zangu wasiniweze wala kunisogelea, nifanye wapekee na vile unavyotaka. Watu wakiniona mimi wakuone wewe Mungu wangu. Wewe ni kimbilio langu siku zote za maisha yangu.
Kitu pekee sijutii kwenye maisha yangu ni kukufahamu wewe, Nakupenda sana Mungu wangu wa mbinguni.Nakupenda.β