
LOML | Love Of My Life (67)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:67
Nilivutiwa sana na maombi haya, anaomba kwa utulivu wakati mimi nilikuwa nalia napayuka nalalamika.
Taratibu niligeuza kichwa changu, nilikutana na uso wa binti huyu mzuri sana, binti ambaye nilikuwa napambana kumtoa akilini kwaajili ya kulinda na kujenga ndoa yangu.
Alikuwa amefumba macho yake machozi yanatoka lakini yeye anatabasamu tu na kutafakari. Mara niliona amefungua macho yake anatazama tu mbele hata na mimi nilitazama mbele pengine kuna kitu. Nilitabasamu na kumtazama nikamsalimia kwa lugha ya kanisani na sauti yangu ya maumivu βMungu ni mwema.β
Kwa sauti ileile ya utulivu alijibu akitabasamu βKila wakati.β
Nilifuta machozi yangu, aliendelea kutazama na kusema βwatu ni watu hata uwafanyie nini, inachukua Musa sana kukutana na binadamu. Pole sana na hongera kwakuwa upo sehemu sahihi.β
Nilitabasamu, yeye akawa anainuka lakini inuka yake alikuwa anapapasa kutafuta fimbo, nilishangaa ina maana ni kipofu. Nilimsaidia na kumpatia fimbo na kumuuliza βnaweza kukusaidia?β
Aliniambia kwa upole βusijali ninaweza.β
Alianza kuinua miguu akitafuta njia, sasa kulikuwa na vitiviti. Nilijikuta naamka nimsaidie. Alitabasamu na kusema βNashukuru sana.β
Nilishusha pumzi na kujikuta nasema βNaitwa Rodricky, niliwahi kukuona kabla na natamani nizungumze na wewe. Tafadhali tunaweza kufahamiana.β
Alikaa kimya kwa muda. Kisha alikuwa kama ananitazama ila ukweli ni kuwa hata haoni. Macho yake yapo Kama anaona vile, na ni mazuri sana. Aliniambia kwa upole βMimi Naitwa Pina.Sina Muda kwasasa naishi mbali kidogo.β
Akawa anataka kuondoka, Nilishindwa kujizuia, hata sijui kwanini nilishika mkono wake kWa upole na kusema kwa huruma β¦πππππππkuna watu wanakujaga kwenye maisha yetu kama majini aiseeeee Ila Gabriella ππππππ
NAAAAAAAAM
HUU NDIO MWISHO WA SEASON ONE