
LOML | Love Of My Life (69)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:69
Pina aliniachia ingawaje mimi nilikuwa natamani hili kumbato liendelee Tena na Tena na tena, nilimshika mkono, yeye uso wake ulikuwa usoni kwangu tu na aliniambia βPole sana Rodricky, nimewahi kuwa kwa hali kama yako, nimewahi kujisikia hivyohivyo. Lakini sasa nipo hapa. Ninatabasamu na ninayo amani.β
Nilimtazama, mara nilisikia Mlio wa simu ndogo hizi nokia torch. Alijipapasa kiunoni, na kisha alipokea na kusema βhello.β
Upande wa pili alizungumza nini mimi sijui lakini yeye alisema βUsijali kabisa bibi, nipo salama. Nitarudi sio muda. Nimekutana na rafiki ananihitaji. Nikizungumza naye nitarudi hapo haraka. Naomba nisamehe sana bibi yangu mrembo kuliko mabibi wote duniani.β
Nilijikuta natabasamu vile anaongea ana furaha sana na tabasamu La kutosha. Na vile amesema amekutana na rafiki anahitaji kumsikiliza. Halafu alipomaliza alikuwa anatabasamu bado akisema βbibi yangu, tunaweza kutoka hapa sasa Rodricky?β
Nilimshika mkono, na hakubisha taratibu tulianza kutoka na nilimuongoza mpaka kwa gari. Nilimfungulia mlango wa gari, nikamsaidia kuingia na kisha na Mimi nikazunguka upande wa pili na kuingia.
Nilimsaidia msichana huyu mzuri kumfunga mkanda na kisha aliniambia βnimekuamini.β
Nilitabasamu na kusema βnakuahidi sitakufanya jambo lolote baya.β
Aliniambia tena βMazingira ni haya haya hakuna kuondoka hapa tafadhali.β
Nilimtazama na kusema βhakuna shida, Hakuna shida kabisa.β
Nilisogeza tu gari ili Ikae sehemu nzuri maana Mungu peke yake ndiyo anajua namna nimefika hapa na kisha nilisimamisha gari. Nikawa tu namtazama huyu mrembo usoni. Alinyamaza kimya tu.