LOML | Love Of My Life (70)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:70
Na kisha aliniuliza β€œRodricky hautaongea utanitazama tu?”
Nilishtuka na kusema β€œIna maana unaniona?”

Alitabasamu na kusema kwa unyonge sana β€œNi mwaka karibia wa nne sasa sioni, lakini nashukuru Mungu nina hisia kali sana ndani ya moyo wangu. Nina uwezo wa kufanya vitu vingi kama mtu anayeona. Tafadhali Unaweza kuniambia una shida gani?. Ni mara chache kwenye maisha yangu kuona mwanaume akilia kama ambavyo umelia leo kanisani. Kitu kibaya kimekutokea.”

Nilinyamaza tu machozi ndiyo yakitoka. Halafu aliendelea β€œUpo kimya na wewe ndiyo ulisema nibaki unahitaji mtu wa kuzungumza na yeye.”

Nilijikuta nasema β€œPina, nisamehe sana kwanza kwa usumbufu. Kusema ukweli wa Mungu sijui hata pale nimefika vipi. Na sijui sasa ningekuwa nimekamatwa hata kwa kesi ya kuua. Sikuweza kujizuia kabisa nilitaka kumuua yule mwanaume mpumbavu na mshenzi Mungu wangu!!, Mungu wangu!!”

Pina alikuwa ni mwanamke mwenye huruma sana, ukizungumza kitu uso wake unakuwa unaonyesha kabisa kuwa hapa anaumia, anajisikia vibaya na anateseka na wewe.

Ana utulivu sana, aliniambia kwa upole β€œMaumivu yanaweza kukufanya ukafanya jambo ambalo kwenye maisha uliwahi kuwaza ni wanyama peke yao wanaweza kufanya.

Maumivu hubadilisha tabia za watu. Najaribu kukuelewa lakini sidhani kama huu ni wakati mzuri unaweza ukanielezea na nikaelewa. Unaweza kutulia na ukaniambia nini kinakutokea Ricky!!!”

Nijifuta machozi, unajua vile sijawahi hata kusema kwa mtu yeyote kuhusu mke wangu ni mara ya kwanza najisikia kufunguka kwa Pina.

Ndipo nilianza kumuelezea namna ilikuwa, nilimuelezea hatua kwa hatua kasoro upande wake tu, nilimuelezea namna nilikuwa namchukulia mke wangu, namna nilianza jifunza kumpenda tabia zake, vitu vyake, na namna lile tukio La ajabu, tulivyo maliza mpaka hospitali na hata haya nimeyaona leo.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata