LOML | Love Of My Life (71)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:71
Niliendelea nikisema huku nalia sana β€œanawezaje Pina. Msimamizi wa ndoa, mtu ambaye alitakiwa kuwa mshauri wangu, muda huu niwe kwake aniambie nini cha kufanya yeye ndiye ana haribu ndoa yangu. Mtu ambaye ni mtu wa karibu na mimi kazini Kumbe ana mfahamu mke wangu zaidi yangu.

Pina, anafanya naye vitu vya ajabu siwezi hata kusema ni nini, nashindwa kukubali kuwa ndoa yangu haikuwa hata na jambo la maana. Unawezaje siku ya ndoa yako, Mc anakuwa yule mwanaume tena ambaye umewahi kuwa naye au upo naye hata aibu unakosa mbele ya mumeo na familia yake unamchoresha namna hiyo.

Ninaumia sana Pina. Maumivu yamejaa hapa kifuani, nyongo chungu inachemka kifuani kwangu na kusababisha sumu ya maumivu kusambaa kila eneo La mwili wangu. Naumia kila sehemu, kila sehemu Pina inauma.

Hapo sijamuongelea Dokta Mungu wangu sijui wametongozana muda gani. Wamefanya kila kitu na kila mwanaume anaongelea namna alivyo mtamu kitandani alivyo fundi inaniuma sana unajua. Zile picha nikiona, meseji zao za ajabu maskini nashindwa hata kuelewa.

Sijakagua simu yote nimeshindwa, natetemeka kuwaza yule ni mke ambaye nimeoa mimi. Hata jehanamu hafai ni kama vile atengenezewe sehemu yake ya kulipia makosa yake ambayo itakuwa na moto mkali zaidi.

Pina unajua kitu kibaya zaidi, nilikuwa nimekubali mimi ni baba, mimi ni baba mtarajiwa lakini nilichokiona mtoto yule ambaye alifanya nimuoe yeye sio wangu, na Kama ana maelezo kuhusu hili basi mtoto mmoja ana baba wengi sana, wengi sana.

Ninaumia natamani uone vile naumia, ninateseka natamani uone vile nateseka. Sikuwa nataka kumuoa mimi, ilinibidi na sasa kumbe nilikuwa natakiwa kulia namna hii.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

JOGGING MASTER FULL

KIBOKO YANGU FULL

KIAPO CHA MASIKINI FULL