LOML | Love Of My Life (73)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:73
Nililia sana, nililia kwa muda na hata nikawa tu napumua kwa nguvu. Na Pina msichana mstaarabu huyu aliniambia β€œtafadhali tulia, tulia tafadhali Ricky, nakuomba.”

Nilimshika mikono yake milaini na kwa upendo nikaikumbatia na kusema β€œnashukuru sana Pina. Sikujua kama nitakuona tena leo, sikujua kama tutaonana.”

Pina alinitazama na kusema β€œulisema umewahi kuniona kabla.”
Nilimtazama kwa upole nikasema β€œndiyo hapahapa kanisani, lakini sikukuona tena?”

Akaniuliza akinishangaa β€œina maana ulikuwa unanitafuta?, kwanini?”
Nilishindwa kujibu badala yake nikisema β€œsijui ila nilikuwa natamani kuzungumza na wewe, siamini leo kama nimezungumza na wewe Pina.”

Alishusha pumzi na kusema β€œRicky, unakumbuka ndani nilisema nini?”
Nilimtazama tu na kisha nilimjibu β€œnikumbushe tafadhali.”

Alivuta pumzi na kisha kwa upole alisema β€œmtu ni mtu tu, siku zote atakuwa hivyo huchukua muda sana mtu huyu kuwa binadamu.”

Nilimtazama na kisha aliendelea β€œkuna watu wanafanya mambo kwasababu tu wameamua kufanya, ndiyo aina ya maisha wamejichagulia. Wanajisikia kupata amani na kufurahia wakifanya hivyo.

Ni hulka zao kamwe huwezi badili au kuzuia ndiyo alivyo. Na wengine ni maumivu yamebadilisha tabia zao na kuona kila kitu ni sawa tu mwenye maisha yao. Lakini kubwa na zaidi watu wengi sana hawana Mungu ndani yao.

Kumkosa Mungu, hata ile hofu ya Mungu kwenye maisha ni mzigo mkubwa sana. Utafanya mambo ya kutisha na utaona kawaida kabisa na wala hutomuelewa mtu yeyote yule akikushauri kuwa unachofanya ni kitu kibaya.

Sitaki nikusumbue na maneno mengi sana Ricky kwa siku ya Leo. Unatakiwa kunyamaza, unatakiwa kujikaza wewe ni mwanaume na ile ni nyumba yako. Rodricky pale ni nyumbani kwako na huwezi kubadilisha kuwa yule ni mke wako lazima mtakaa pamoja, lazima mtazungumza.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

BIOLOGY TEACHER FULL

KIAPO CHA MASIKINI FULL

BINTI MDUNGUAJI FULL

SHEMEJI UMECHOMEKA KWELI? FULL