
LOML | Love Of My Life (74)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:74
Kitu pekee unatakiwa kujua ni kitu gani unafanya, familia zetu zitasema nini, kumbuka ni ndoa Rodricky ni ndoa. Sio kitu tu ambacho utajiamulia wewe peke yako ndani ya ndoa hiyo unayoona haifai wapo watu wengi mpaka serikali inahusika na kΔ±la mtu hapo hatamani mtengane.
Sasa Naomba nisikie, binadamu huwa tunajikita sana kwenye kuomba jambo fulani tu kwa Mungu na kusahau kuwa hata haya magumu Mungu ameyaruhusu kwasababu.
Upo ushindi mbele yako na ili ufike hukuwa na namna ya kukwepa hapa. Mshukuru Mungu kwa yote aliyokutendea, kwa biashara yako, kwa familia yako, kwa maisha yako, kwa mke wako, kwa marafiki, kwa nyumba, kwa gari, kwa kΔ±la kiti kinacho kuzunguka na mwambie Mungu akupe hekima kama Selamani.
Kupitia hekima utayaweza yote kazini, nyumbani na popote. Neno la Faraja nitakupa ili upate nguvu ya kuvuka hapa, beni ambalo hata mimi binafsi limenifikisha hapa.Wafilipi 4:13 Naweza kufanya mambo yote katika yeye anipaye nguvu.
Mungu peke yake, ndiyo anaweza kukufanya ukashinda Vita yako. Ukaona hili ni jepesi na ukafanya maamuzi ya busara na yenye amani kwenye maisha yako.
Eenh kuna zaburi 23:4 Nijapopita katika bonde la giza kuu la kifo, sitaogopa hatari yoyote, maana wewe ee Mwenyezi-Mungu u pamoja nami; gongo lako na fimbo yako vya nilinda.
Rodricky, unaonekana ni mtu mzuri, usikubali hasΔ±ra yako ikutenge na Mungu. Jizuie, ongea na Mungu, kuwa mpole, jitie nguvu, kuwa imara, sikiliza ndani yako wewe unataka nini. Hizi kugombana, hizi kutaka kuua utaishia pabaya.
Huna sababu ya kuhangaika na yeyote. Muachie Mungu atahangaika nao. Tulizana, tulizana na ufanye mambo kwa usahihi. Mwisho wa siku utaonekana wewe ndiyo una shida ndani ya ndoa yako na Kumbe sio wewe, jikaze kiume, pambana na mke wako yeye ndiye shida, Hakuna mwanamke mwenye upendo na mume wake atafanya hayo anayofanya, Mpe sikio Labda anayo sababu ya hayo japo sijui kama kuna sababu ya kuhalalisha haya.