LOML | Love Of My Life (75)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:75
Lakini Sitamani ufanye kitu kibaya kiukweli ambacho kitakudhuru wewe au mwingine. Unaweza, wewe ni mtu mzuri Rodricky.

Tafuta muda wa peke yako, tafakari, fikiria na mwisho wa siku utapata majibu ya nini unatakiwa kufanya. Nakuomba tafadhali.”

Mimi nilikuwa namsikiliza kwa utulivu namna anazungumza ni kama awe anazungumza tu. Unajua kuna watu wanaongea kwa upole na upendo mwingi kiasi kuna muda unaacha kusikiliza vitu anaongea unaanza tu kumtazama usoni. Alikuwa na upendo mwingi, na upole wa kutosha na ni mtu mwenye utulivu sana.

Alinitazama na kusema β€œnatakiwa kuondoka sasa Rodricky.”
Nilimtazama na kusema β€œPina, naweza kukukumbatia tena?”

Alitabasamu, na Mimi nilifanya hivyo kwa upendo na Kisha nilisema β€œnashukuru sana, Asante sana Pina. Mungu akubariki sana. Baada ya kuzungumza na wewe walau Nina amani na utulivu kiasi ndani yangu. Nakuahidi sitafanya kitu kibaya. Nakuahidi.”

Alitabasamu na kisha alisema β€œMungu akuongoze, jiweke karibu na Mungu. Atakupa sababu kumi elfu za kuwa na furaha hata mambo yakiwa magumu zaidi jua Mungu yupo hapo kuna mahali anataka ufike. Wewe ishi tu.”
Nilitabasamu, alitabasamu na kusema β€œnaweza kushuka sasa.”

Nilisema kWa upole β€œnashukuru sana, ninaweza kukupeleka Naomba usikatae.”
Alifikiria kwa muda, Kisha alisema β€œNi Sawa hakuna shida.”

Kisha alinielekeza anapoishi, palikuwa na umbali kiasi na nikamuuliza β€œIna maana huwa unatoka huko kwani hakuna kanisa huko?”

Alitabasamu na kusema β€œlipo lakini na hata mimi sijui kwanini Napenda kuja huku nafurahia zaidi mahali hapa ni kwasababu labda ninayo hadithi nzuri kuhusu mahali hapa.”

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

KIBOKO YANGU FULL

UTAMU WA JAMILA FULL

TOBO LA PANYA FULL